G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,593
- 36,010
Kwanza kabisa nieleze masikitiko yangu kutokana na hotuba ya jana aliyotoa rais Magufuli akizindua mwaka mpya wa mahakama! Rais alidiriki kuwaeleza majaji na mahakimu (siyo mawakili) ambao ndiyo waamuzi wa haki kimahakama eti wafanye juu chini waamue mashauri zaidi ya 400 kwenye mahakama zao ili serikali ipate trilioni moja ambapo amewaahidi robo ya fedha hizo! Kwa maana nyingine rais anawataka majaji kuwa ni lazima serikali ishinde kesi zote ili wanufaike! Hili ni jambo la ajabu sana kusemwa na mkuu wa nchi tena huku akiwaelekeza majaji kufanya hivyo!
Rais Magufuli anajua uzito wa kauli ya mkuu wa nchi? Anategemea nini kutoka kwa majaji hawa kuhusu haki? Jambo la zaidi ni kuwa rais ameshawishi haki kwa kuahidi rushwa!
Wiki ijayo mwishoni Magufuli anatimiza siku 100 rasmi akiwa ikulu! Tuna kumbukumbu ya sakata la bomoa bomoa! Uachishwa kazi kwa watumishi wakubwa serikalini bila ya kuwepo maelezo ya kina kuhusu makosa waliyotenda! Tuna kumbukumbu ya Alphonce Mawazo kuuawa kinyama huku serikali yake ikiwa haijatilia maanani uzito wa jambo hilo!
Yote kwa yote sakata la Zanzibar hajawahi kulitolea msimamo zaidi ya kupokea kauli kutoka kwa wasaidizi wake huku mambo yakiendelea kuharibika waziwaizi!
Utawala wa rais Magufuli unaonekana kuwa utawala unaotaka kulazimisha matakwa yake yaende hata pale inapoonekana kuwa siyo sahihi! Mwisho wake wapo wengi wasio na 'meno' wanaoathirika kwa kiwango cha juu! Mfano utawala huu umedhamiria kupata hela ya watu wake kwa gharama yoyote ile mfano kusitishwa uonyeshwaji live wa bunge ili kupata bilioni nne za wananchi! Kwa dhana ya utawala wa watu siyo sahihi hata kidogo! Hata hili la kesi za trilioni moja, tayari maslahi ya kupenda hela kupita kiasi yameonekana dhahiri! Kwa stahili hii ataongeza mishahara ya watumishi kweli?
Jambo lingine inaonekana Magufuli tayari amekuwa na mashaka na watendaji wake kuwa ikiwa ataenda nje ya nchi basi mambo hayataenda! Yaleyale ya rais kuwa kila kitu na kila tamko! Kitendo cha rais Magufuli kushindwa kuhudhuria mambo muhimu ya kimataifa kama kiongozi wa nchi kisha akamtuma makamu wa rais ama waziri mkuu hakijengeki hoja ya kubana matumizi kwani kitu ni kilekile! Hapa lipo tatizo eidha kwa niliyoyasema au lipo jambo lingine!
Kumbuka kuwa nchi yetu ni kweli inahiaji rais 'mkali' lakini rais huyo ni lazima aelewe kuwa kuna swala la utaifa, haki na utu wa kila mmoja! Kuna marais wengi duniani ni wakali lakini kuna aina ya ukali inayotakiwa ingawa hapa nashindwa ni namna gani niielezee!
Maoni: nchi yetu wasaidizi wa rais wajifunze kukosoa hadharani pale inapotakiwa kufanya hivyo mfano Jaji Othman Chande jana hakutakiwa kukaa kimya baada ya rais kutoa maelekezo tata kiasi kile! Kukemea kuwe sehemu ya utamaduni! Nadhani ndo maana wasaidizi wengi wa Kikwete wameonekana wazembe baada ya yeye naye kuonekana mzembe! Hali hii inatokana na umungu mtu wa marais wetu! Kila rais anaonekana kuwa na hulka ya utawala wake huku wasaidizi wake wakipelekwapelekwa tu bila kuhoji na kukemea! Ndo maana wakina Lukuvi na Makamba, Ummy na Majaliwa, Kigwangalah na Maghembe wa Kikwete wamekuwa tofauti kabisa na hawahawa wa Magufuli! Umungu mtu wa rais! Kwamba Kikwete alikuwa hivi na ni lazima wasaidizi wawe hivi! Magufuli yuko vile na ni lazima wasaidizi wawe vile! Hii ni hatari kwa nchi! Hasa pale rais anapokosea na wasaidizi wake wasiweze kuhoji!
Tunajua kuwa wapo ambao hawataki kabisa Magufuli kukosolewa! Wao wajiulize tunakosoa kwa halali?