Baada ya siasa kuisha kazi ubungo imeanza

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Kwa wale ndugu za ngu wachagga waliozoea kuwa Moshi kwao saa sita mchana biashara hiyo imesitishwa kwa muda kutokana na madereva wa mabsi waliokuwa katika mgomo kuamua sasa kuwa watiifu wa sheria kwa kuendesha mabsi kwa kilimota 80 kwa saa, pale kwenye vibao vya 50 na 30 ni lazima kuvizingatia.

Mbasi yanafika Mbey saa nne usiku, Mwanza saa sita au saba usiku, Dodoma saa tisa mchana n.k. Abiria wanakaa mapaka makalio yanauma na wanasimama hadi trafiki wanafikiri mabasi yamezidisha abiria kumbe la?

Tochi za trafiki hazina kazi sasa. Nasikia upo mpango wale wote walio natochi barabarani watapangiwa bunduki wakalinde mapori ili mabsi yasivamiwe na majambazi kutokana na kulazimika kutembea usiku. Ubunifu Mzuri au sio?

Chama cha madereva wa mabsi UWAMATA kinahakikisha kuwa kinapanga wakaguzi kila njia kudhibiti madereva wakorofi. Zoezi hilo limeanza kuonyesha mafanikio baada ya Serikali kuamua kuruhusu mabsi yenye chasisi za maloro kufanya kazi na hivyo wamiliki kujiepusha na hasara.

Mwanzoni wamiliki walikuwa wakinufaika kutokana na speed za madereva. Hivi sas baada ya kibano cha serikali kutokana na wamiliki kuunga mkono mgomo wa madereva kisirisiri kwa kutochukua hatua zozote wamebuni mpango huu na kuuwapachikia madereva ili uonekana ni wa madereva na ili kuishawishi serikali iwasamaehe waendele kutembeza chasis za maloro kama mabasi.

Bravo wamiliki this is bongo!!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom