Baada ya miaka kadhaa Afrika tutakuwa tunafikiri sawa

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,208
14,137
Zamani tulikuwa na mbegu nyingi tofauti za mahindi, sasahivi aina Moja au mbili ya mbegu zinauzwa na kujaribu kulazimishwa kupandwa nchi nzima.

Tulikuwa na aina nyingi za kuku wa kienyegi, Sasa ni kuku wa kisasa na mayai ndio mfumo Mmoja.

Tulikuwa na ng'ombe wa maziwa aina nyingi Sasa kila mahali wanatakiwa wapandikizwe mbegu Moja.

Hata matunda, nyanya na mbogamboga siku hizi mbegu ni za aina Moja hivyo soon tutajakula embe LA aina Moja.

Kilimo cha samaki nacho kinashika kasi na mbegu itakuwa ni Moja tu.

Hivyo tutakuwa tunakula vyakula vya aina Moja na ambavyo ni kutokea Maabara.

Tuje kwenye malezi ya Watoto,
Sasahivi zimefunguliwa Child care nyingi ambazo unapeleka Mtoto wewe ambaye Huna time na watoto wako. Huko wanafundishwa tabia za aina Moja na wanapewa malezi ya aina Moja. Hawa wakikuwa wakubwa watakuwa na tabia za aina Moja yenye malezi ya aina Moja. Baada ya miaka kadhaa kinatokea kizazi chenye tabia Moja, Ufikiri wa aina Moja, mienendo ya kimaisha ni aina Moja na hata namna ya kutatua matatizo itakuwa ni ya aina Moja.

KWA HAYO YOTE KWANINI TUSISEME BAADA YA MIAKA KADHAA TUTAKUWA TUNAFIKIRI SAWA?
 
Hatuwezi kufikiri sawa kwasbb tunatumia vya kwao. Tungekuwa tunaboresha vya kwetu afadhali. Kufikiri sawa ni hatua ndefu sana mkuu. Hebu umiza kichwa mkuu. Kutumia kila kitu cha mzungu haimaanishi tutakuwa tunafikiri sawa.
Siyo km napinga lkn kufikiri sawa ni hatua ndefu sana.
 
Hakuna kitu kama hicho.

Kuna nature na nurture, miongoni mwa watu kuna tofauti nyingi hasa za kurithi kuliko za kimalezi.
 
Back
Top Bottom