Baada ya mechi ya Ruvu shooting, Zahera afunguka haya

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,407
36,551
NUKUU ZA ZAHERA LEO JIONI.

- Timu yangu imecheza ovyo sana lakini nashukuru tumepata ushindi.

- Jana ilikuwa dirisha dogo la usajili linafungwa ni siku ambayo uongozi wa Yanga umefanya vitu vya ovyo sana.

- Nilifikiria kuwaachia timu yao , ila nikambuka jinsi wanachama wanavyoipenda timu yao nikaamua kubaki.

- Sipo Yanga kwa ajili ya pesa, nipo kwa ajili ya kuipambania timu hii kutokana na mashabi wanavoipenda timu na ushirikiano wanaonipa.

- Siku ya Alhamisi niliambiwa wamewasainisha tayari Mshambuliaji wa Uganda, kipa wa Kenya na winga wa Mwadui. Niliwapongeza kwa hilo.

- Jana usiku saa 5, napigiwa simu na mshambuliaji mganda kuwa amesaini Egypt nikawauliza viongozi wa Yanga wakanijibu wamefanikiwa mchezaji mmoja tu ambaye ni Haruna Bobani.

- Tulikubaliana kuwa mzunguko wa kwanza tusifanye usajili mkubwa, ila dirisha dogo tusajili walinipa masharti kuwa niwe nafasi ya pili au tatu.

- Kwa mambo haya wanayofanya, nisiulizwe kuhusu ubingwa wala nikipoteza mchezo dhidi ya Simba maana viongozi ni wababaishaji.

- Reuben Bomba ni mreno pia ana uraia wa Congo ni mchezaji mzuri sana, na tulikubaliana apewe mkataba wa miezi sita, kwa kuwa alikuwa anaenda ulaya na alikuwa anasubiria viza yake, lakini nashangaa kwenye mitandao viongozi wanadai mimi ndo nimemkataa. . ntamkataa vipi mchezaji mzuri kama yule.

- Timu haina hela wachezaji wana matatizo mengi na hawajui lini watalipwa lakini wanacheza kwa moyo wote, angalia Makambo hajalipwa hata sent ya usajili na juzi hapa mizigo yake ilizuiliwa hotelini kwa kuwa hajalipa gharama za chumba.

- Niliwaambia waniletee kipa wa Kenya, wanasajili kipa hata simfahamu na wala sikumpendekeza hata sijui anaitwa nani na anatoka wapi hii ndo huwa naita kitu ya ovyo.
 
mpira wa Tanzania haukui kwa sababu ya viongozi wababaishaji kama hawa wanaomba uongozi kazi hawawezi.
Zahera anatakiwa awe mkurugenzi wa ufundi na kocha
Ila nawapongeza waliobuni mpango wa wanachama kuwapa pesa moja kwa moja kocha na wachezaji kila baada ya mechi kuwaruka viongozi wenye tamaa ya ela
 
mpira wa Tanzania haukui kwa sababu ya viongozi wababaishaji kama hawa wanaomba uongozi kazi hawawezi.
Zahera anatakiwa awe mkurugenzi wa ufundi na kocha
Ila nawapongeza waliobuni mpango wa wanachama kuwapa pesa moja kwa moja kocha na wachezaji kila baada ya mechi kuwaruka viongozi wenye tamaa ya ela
Zahera anapata nguvu toka kwa mashabiki
 
hahaha yan anachoogopa huyu kocha ni kufungwa na simba tusimba ipo nafas ya 3 ila bado anaiwaza cjui kwann, kwann asiizungumzie azam iliyo nafas ya pili?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Jamaa lazima aiogope Simba,maana lazima Yanga alale round ya pili baada ya kunusurika round ya kwanza.Zahera analijua jambo hili vyema kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom