Baada ya madereva wenye vyeti fake kutimuliwa Ajali za STK, STJ, SU na DFP zimeshamiri

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
Kwa utafiti mdogo niliofanya ndani ya miezi hii mi 2 ajali zaidi ya 5 zimetokea zikihusisha magari ya SU, STK, STJ na DFP mengi kati ya magari haya yamepata ajali usiku na yanaendeshwa na madereva wapya baada ya wale wazoefu kutimuliwa kwa vyeti fake.
Tatizo linaweza kuwa nini? Nilitegemea perfomance yao ingekuwa juu sana maana wana vyeti original.
 
Ni kweli hata Mimi Niko taasis flani nyeti tu. Dereva mzoefu kaachishwa. Akapew gari dereva mpya tens form six. Beta, NIT.Na ufundi juuu. Kwenda Arusha tu. Gari kurudi utadhani lilishambuliwa Na vifaru! Maana Lima mibonyeo kila kona, taa za nyuma tens upande wa dereva zimevunjika!!
 
nina bachelor degree ya masuala ya biashara hadi sasa nimepata ajali saba nne kati ya hzo ni kubwa

Nina mjomba wangu ni darasa la saba anaendesha gari huu ni mwaka wa 25 hajawahi kupata ajali hata moja na yy ni mpiga masafa marefu

serikali kwenye hili hawakujua kuwa cheti cha form 4 hakisaidii kucontrol gari bali ni dereva ndio anacontrol gari bila kujalisha kiwango cha elimu..

kuna jirani yangu ana PHD ila anaendesha gari kama mwehu vile
 
nina bachelor degree ya masuala ya biashara hadi sasa nimepata ajali saba nne kati ya hzo ni kubwa

Nina mjomba wangu ni darasa la saba anaendesha gari huu ni mwaka wa 25 hajawahi kupata ajali hata moja na yy ni mpiga masafa marefu

serikali kwenye hili hawakujua kuwa cheti cha form 4 hakisaidii kucontrol gari bali ni dereva ndio anacontrol gari bila kujalisha kiwango cha elimu..

kuna jirani yangu ana PHD ila anaendesha gari kama mwehu vile
mkuu nina maswali mawili unisaidie!
1.Hiyo degree yako ya musuala biashara ulifundisha na udereva na ni chuo gani?
2.PHD ya udereva inatolewa chuo gani?
 
mkuu nina maswali mawili unisaidie!
1.Hiyo degree yako ya musuala biashara ulifundisha na udereva na ni chuo gani?
2.PHD ya udereva inatolewa chuo gani?

madereva waliofukuzwa walifukuzwa kwa sababu ya vyeti vya form 4 ndio vilikuwa na tatizo lakini NIT walienda na kusoma hizo kozi za udereva

my point was kuwa na cheti cha form 4 au hata 6 hakukufanyi kuwa dereva mzuri...

kunakokufanya kuwa dereva mzuri ni kozi ya udereva na wew dereva mwenyewe sasa kutumia kigezo cha vyeti vya form 4 kwa madereva matokeo yake ndio haya mwisho wa huu kwenye minada ya bima salvage za serikali zitakuwa nyingi sana kwa sababu vya hivyo vyeti vya form 4 walivyovitaka
 
Kuna ukweli katika hili. Nafanya kazi kwenye insurance industry. Ukisoma taarifa ya Police-PF 90 inayo onyesha maelezo ya ajali hasa details za Gari na Dreva, utakuta madreva wengi wana miaka kati ya 24- 27. Ni vijana kabisa kwa maana halisi ya neno hilo. hawana uzoefu barabarani. Hata Dreva aliyewaua wafanyakazi watatu wa TIC nadhani alikuwa na miaka 27 tu. Anakutana na paka Barabara badana ya kumgonga, yeye anakimbilia porini....Uzoefu barabarani wakati fulani ni zaidi ya cheti....na watawaua sana....
 
Kuna watu MNA akili sana. Huu ndo utafiti wa kuleta jamvini. Hata kama COSTEC wakikunyima kibali wananchi tunakupa kibali. Serikali ya zimamoto haiwezi kujua haya. Mtu mmoja akiamka asubuhi kagombana na mkewe anakuja na maamuzi ya kipuuzi Kama hayo ya kulazimisha dereva awe form IV! Na bado, magari ya serikali yataangushwa sana kwa upumbavu wa mtu mmoja. Mkuu wa usalama barabarani kafuata midundo ya mihemko kakurupuka kila dereva atembee na cheti, ameona amechemka katoa miezi 5 madereva wakasome. Kama hivyo vyeti ndio ubora wa udereva kwa nini wameruhusiwa kuendesha bila vyeti? Si wangeambiwa hakuna kuendesha hadi uje na cheti? Yaani wameruhusu mtu asiye mtaalamu afanye Kazi ya kitaalamu(kwa maoni yao) wakati bado anasomea huo utaalamu!!?
 
Back
Top Bottom