Baada ya Kurudishwa Kutoka Marekani.

Kimsingia mimi ama wewe ndo waamuzi wa maisha tunayoishi, either uishi bongo, au ng'ambo, maisha yako ni vile utakavyoamua
Kuna jamaa flan ambao wanaishi bongo na ng'ambo na huwezi ona tofauti yao maana wao wako kwa ajili ya maisha na plan zao
kuna ambao either walirudi ama kurudishwa still wakafika bongo wakayapatia maisha na hawajutii kurudi bongo
Kuna jamaa wengine waliporudishwa wamejikuta wakishindwa life la bongo wengi wamebakia kuwa walevi,wasiojishughulisha na ambao wanaishi maisha fake, wako bongo ila tabia za kimtoni mtoni
all n all mimi au wewe ndo wapangaji wa maisha yetu
 
Hivi 'elimu' ni nini? Inapatikana wapi? Uzoefu unaweza 'unaelimisha'?
 
Hata kama ni over 45, bado fursa ya kupata elimu/ujuzi wanayo na wanaweza kufanikiwa sana kimaisha. Watu huwa wanafanya makosa. Kizuri ni kujifunza kutoka kwenye hayo makosa na kuyafanya ni daraja kufikia mafanikio.
 
Aminiusiamini! kama wenzio walikukaribisha huko USA na mkaishi kama ndugu, ni jukumu lako kuwatafuta na uwasaidie hata kwa kuwapa moyo na ushauri jinsi ya kuishi. Huenda wakafanikiwa na wakakusaidia tena!
 


Mkuu umenena hasa hapo kwenye bold.
 
wapo wengi tu bongo tunawaona..visista du vinashoboka na kiingereza cha kimarekani..kumbe njemba ishaiba texas imesepa..ipo bongo inakula faida..
 
Topic sijaipenda hii !!
unavoanza nilijua sijui unataka kuelezea jambo fulani la maana, ****zako !!!
 
Topic sijaipenda hii !!
unavoanza nilijua sijui unataka kuelezea jambo fulani la maana, ****zako !!!

Punguza jazba ndugu, matusi hayakusaidii kama ulikuwa huna cha kuchangia ni bora ungempotezea tu.
 


hivi wewe unajua gharama za kujisomesha marekani au unasema tu?,uliza kwanza.
 
wapo wengi tu bongo tunawaona..visista du vinashoboka na kiingereza cha kimarekani..kumbe njemba ishaiba texas imesepa..ipo bongo inakula faida..

ni bora hata huyo aliyeiba na kurudi nyumbani, at least he did something.
 
Yooote tuandike hapa....Lakini cha msingi hawa jamaa wanahitaji msaada. Umeshapanga namna ya kuwasaidia hawa rafiki zako. Tuache blah blah wakati watu wana shida.
 

Nakataa siyo lazima. Inawezekana nakuzidi mshahara wakati nina certificate tu. Acha itikadi za kizamani. Bakhresa ana degree? yuko wapi?
 
mkuu ulichonena kina ukweli, ila jamani ndugu zetu mliopo ng'ambo kumbukeni kujenga walao kibanda huku home, mambo yanapokua mazuri huko na sio kula bata tu, kuna jirani yangu hapa kakaa usa 17yrs, karudi kafikia kwa kaka yake, hana chochote, kila siku pombe na sasa kesha anza kunywa na zile za kienyeji, hii thread imenigusa sana, maana inaonekana kuna tatizo, si bure kwa hawa ndugu zetu walio ng'ambo licha ya kwamba si wote
 
maisha ni mipango na malengo, kupanga ni kuchagua ikumbukwe kuwa si kila upangapo au uchaguapo jambo basi litakuwa hivyo.
haya nayo yamo.
 
nawasihi sana wale waliopata fursa kuzitumia kwa maana na umakini na malengo yaletayo manufaa kwa sasa na badae. hao jamaa hatuwezi kuwasemea sana kwa sababu hawapo hapa tukasikia nini wao wangesema. kama walifikiri hawatarudi home kabisa au walikuwa na sababu gani za kukutwa na yote haya.
ila mliopo huko sasa elimu ni muhimu, kuweka akiba ni muhimu sana. wajipange wasijekutwa na mambo kama haya.
japo kufanikiwa katika maisha si kuwa na elimu tu, kunahusisha na mambo mengi.
 
angalia wazungu wakija bongo wanahakikisha wanachota vya kutosha vijiopportunity vikijitokeza wanachangamkia na hata wakirudi kwao wanachakuanzia ama waweshajiwekea akiba kubwa. kwa watu ni kwa watu tu. panga mipango mizuri kwenu hata kama hutarudi milele unaweza ukawa umewekeza vilevile. kikawa moja ya chanzo cha mapato vijisent hutakosa.
 
Marekani na kwingine watu wanaenda na kazi zipo!! Kuna makundi ya watu tena ada wanatumiwa lakini hawakusoma na wametesa wazazi wao sana!! Matokeo yao wameishia kubeba maboksi tu na shule hakuna na wakipata hela ni partying tu. Kuna wengine wanaenda wanasoma na maboksi wanabeba ili kujiongezea kipata na maisha yao ni mazuri tena sana!! Kuna wengine wanatafuta njia ya kufika marekani hasa kwa kutumia shule fake, wakifika kule wanabeba boksi na wakipata hela wanasoma!! Bravo!! Wengine wanaenda pale wanaishia kubeba boksi na wakipata hela wanatanua tu hakuna savings, no investments at home!! Yaani nothing!! Sasa wale ambao wanaenda nje hasa marekani ambako opportunity za kazi za vibarua vipo na wanatanua na siku ya siku wanapigwa PI sasa unataka tuwaonee huruma!!! Katika maisha kila mtu atavuna alichopanda!!! No sympathy!!!!!!
 
Halafu usivyokuwa na aibu, unakuja kuwananga hapa ili iweje.

Wamekusaidia wakati ukiwa unahitaji msaada kwa kuwananga hapa kwa akili yako ndiyo unawasaidia.

Binadamu wengine sijui tumelogwa vile

Ndugu yangu, maisha ni kama mlima, usifikilie kwa nafasi uliyonayo umeishafika kileleni. You have a long way to go...

Think bigger.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…