Baada ya kukamilika siku 14 za msamaha kwa wahujumu, Je Rais Magufuli atumie busara za Harun El Rashid kuwasamehe ambao hawakuandika barua? Au...!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,639
Wanabodi,

Zile siku 14 za msamaha wa rais Magufuli za kuandika barua kukiri makosa na kuahidi kutorudia tena na kulipa walichoiba zimekamilika. Ofisi ya DPP imeishaanza kuzifanyika kazi kwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani ili kuisajili misamaha hiyo kimahakama, kwa barua hizi kupokelewa mahakamani kama uthibitisho wa kukiri kutenda kosa, mahakama itatoa hukumu ya kiasi fulani cha faini ya makosa hayo, mtuhumiwa akilipa faini hiyo anaachiliwa na kuendelea kulipa lile deni alilosababisha kidogo kidogo kwa utaratibu watakaokuwa wamekubaliana na DPP. Hivyo watuhumiwa wenye cash cash ya ukweli, kuanza kuanza kuachiliwa anytime from now maana barua hizo zimeanza kuwasilishwa mahakamani siku ya jana.

Hoja ya bandiko hili ni ni kwa wale ambao wana kesi za uhujumu na utakatishaji fedha, lakini hawajaandika barua za kukiri makosa na kuomba msamaha. Jee kutoandika barua huko ni uthibitisho kuwa wamebambikiwa?. Jee tuwaombee msamaha kwa rais Magufuli atumie uadilifu wa Harun El Rashid kuwasamehe?.

Uandilifu wa Harun El Rashid katika kushughulikia mashauri, nimeuzungumza hapa

Lakini kwa faida ya wale wavivu kufuata links, ninakuwekea hapa kisa kimoja cha Mwanamke Tajiri na Mwanamke Masikini kilichoamuliwa na Harun el Rashid.
Katika wahujumu na watakatishaji fedha, kuna makundi matatu ya watu na aina tatu za wahujumu.
Tukianza na makundi ya wahujumu, kuna wahujumu wakubwa, matajiri wenye uwezo wa kulipa chochote. Kuna wahujumu wa kati ambao ni watu wa kawaida, na wahujumu wadogo, masikini wa kutupwa hata wakiandika barua za msamaha, hawana uwezo wa kulipa chochote.
Tukija makosa ya uhuhujumu ya kuombea msamaha
1. Kuna Wahujumu kweli na watakatishaji kweli pesa, hawa wataomba msamaha na pesa wanazo na watalipa pale pale watakuwa huru.
2. Wahujumu waliohujumu kidogo na kubambikiwa kesi kubwa, hawa pia wataandika barua na kulipa kulipa kidogo kidogo.
3. Waliobambikiwa kesi za uhujumu, kwenye kundi hili la waliobambikiwa, nako kuna makundi matatu yake.
1 Waliobambikiwa lakini ni matajiri, hawa wataandika barua na kukiri uhujumu ili tuu kuununua uhuru wao kwa gharama yoyote, hawa watalipishwa na watalipa ila kwa vile wamelazimika kukubali tuu ili wawe huru, fedha zao zina bad karma ya malipizi, Mungu atawalipia.
2. Kuna waliobambikiwa ni watu wa kawaida na wengine ni masikini, hawa pia wangetamani kuandika barua wakiri watoke na wengine watakuwa wameandika barua kukiri kwa kusisitiza kuwa wamesingiziwa, ili watoke, lakini pia watakiri kuwa wangekuwa na fedha pia wangelipa, hawa pia wanapaswa kuachiwa bila kulipa chochote.
3. Kundi la tatu, hawa ni watu wakweli, ambao wataamua kusimama na ukweli mpaka mwisho kuwa wao wamesingiziwa, sio wahujumu, hawataandika barua za kukiri makosa ya kubambikiwa, au wakiandika sio kukiri bali kusisitiza wamesingiziwa, hawa ndio Mungu atasiimama nao.

Sasa kwa kuutumia uadilifu na busara kama za Khalifa Harun el Rashid, jee tumuombe rais Magufuli atumie huruma yake na busara zake kuwasamehe kwa kumuelekeza DPP (japo DPP hatakiwi kuelekezwa, siku hizi DPP anaelekezeka!), kutumia powers zake za Nolle kwa kuwatendea haki watu hawa waliobambikiwa kesi za uhujumu kwa kuzifuta kesi zao?.

Kama nilivyo sisitiza wakati wa kumpongeza rais Magufuli kwa uamuzi huu, naendelea kusisitiza rais Magufuli akitenda haki, yeye atabarikiwa na taifa litabarikiwa. Hawa watu waliobambikiwa kesi za uhujumu wakati kiukweli kabisa sio wahujumu, nao watendewe haki.

Hivyo tumuombe rais Magufuli, aombe kupewa majina ya wahusika wote wa kesi zote za uhujumu aangalie ni wangapi hawaja andika barua za kukiri na kuomba msamaha?, then hao wote ambao hawajaandika barua, ndio watakuwa wamebambikiwa, ili ikimpendeza, ndipo amuelekeze DPP, hao wote waachiwe kwa Nolle, watakuwa ni kweli wamesingiziwa na wakiachiwa watakuwa wametendewa haki.
Mungu mbariki rais Magufuli,
Mungu ibariki Tanzania.
Paskali
 
Amegoma kutoa majibu ya uvumi wa kumchoma kabendera, kwa hiyo kila mtu aamini kivyake
Ila uzi ambao umeweka kama nusu saa iliyopita, ni mwanajf analalamika kuwa watoto wa Pasco wa kiume wana tabia ya kuzalisha wanawake ovyo ovyo halafu wanakimbia kutoa matunzo. Sasa mleta uzi alikuwa analalamika kuwa Pasco anaweka mabandiko ya maana hapa JF lakini ameshindwa kudhibiti wanae wasiwatie mimba wenzao ovyo ovyo
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁
 
Kama wanawake wanajipeleka wenyewe na kijana wake ni mzima afanye nini sasa, hata ingekuwa mimi ningekaa kimya tu
 
Oh! Sasa nimeanza kuelewa, kumbe haikuwa Plea bargain kama sheria inavyotaka. Ilikuwa amnesty for economic saboteurs ila tofauti na amnesty nyingine hii inabidi ulipie. Kweli kama taifa tumesonga mbele, hii nchi lazima iende mbere.
 
Mkuu Pascal Mayalla nashukuru kwa bandiko lako. Naomba niulize maswali machache:-
1. Hivi hao watuhumiwa waliokiri makosa yao wakishindwa kulipa hizo pesa (By Installment) kama walivyokubaliana na ofisi ya DPP watarudishwa mahakamani

2. Hivi kumbukumbu za kimahakama baada ya watuhumiwa kukiri makosa ya mashitaka yao zitakuwa vipi? Je zitaonyesha kwamba wahusika walikuwa wanashitakiwa kwa mashitaka ya kuhujumu uchumi na kushindwa kesi?

Ahsante
 
Bandiko zuri Sana Ila sio wote ambao watakataa kuandika barua ni kuwa hawajafanya hayo Kuna wengine wamefanya hayo na wakapokea Chao wakatumia vibaya sasa hata wakiandika barua watalipa nn?

Na Kuna wale kwa kutaka kujifanya wasafi ktk jamii wakati wamefanya hayo nao wamekataa kuandika barua na sio lazima kuandika barua na wamechangua njia Yao.

Hivyo kwa wote ambao hawakuandika barua kesi zao zitaendelea vile vile na mahakama ndio mwamuzi wa mwisho kama wana makosa au la.
 
Kama utaratibu wa kukamata MTU kumshtaki ungekuwa ni baada ya upelelezi kukamilika. Au ile sheria kwamba DPP akimuweka mtu ndani upelelezi ukamilike ndani ya Siku sitini ingeheshimiwa basi ni wazi hata Leo hii hata waomba msamaha wangekuwa wachache sana.
Lakini haya mambo ya kusota miaka mitano eti uchunguzi bado hakuna anayekubali
 
Naomba link ya hilo bandiko, umri wa mtoto Kitanzania kwa maana ya minor ni under 14, the age of majority kwa Tanzania ni 18 years. Hao wanaoitwa watoto ni watu wazima wamemaliza vyuo vikuu, wanakaa makwao na wana maisha yao, they are adults na wako responsible kwa maisha yao.
P
 
Aliwapa siku 7, akaongeza 7 zingine kwa kuwahurumia. Unashangaza kutaka achukue atua zingine, kama vile hao wahusika hawakupewa nafasi ambayo alisema hatairudia tena. Kwa sasa wapambane na uamuzi wao tu. Kuna walioiba kuku na maziwa na vitu vidogo wapo jela na hata waliosingiziwa kesi. Bora awaangalie hao sasa kuliko hao walioiba pesa nyingi, na ambazo bado wanazo wanavizia mahakama itaamua nini.

Ushauri wako huu akiufata, atajishusha sana. Kuna mengi zaidi ya yeye kutoa nafasi kwa wananchi wengine na yanayowakabiri.
 
Kesi zimepungua sasa uchunguzi uharakishwe na mahakama itoe haki kwa watuhumiwa.

Vyombo vya uchunguzi vimerahisishiwa na kupunguziwa mzigo, sasa wachunguze zilizobaki na kesi ziungurume.
 
Sheria zetu zinaupofu mwingi sijui kazi ya mwanasheria mkuu halioni hili.Jela ni nyumbani kwa kila mtu Leo kwao kesho kwake,sawa na dikteta bashir kulalamika ubovu Wa gereza alilopo hali angewezafanya kitu.Huu utaratibu wa kumkamata mtu mahabusu aoze ndani kwanza ndo ushahidi utafutwe ni Wa wapi huu ni sheria au ni mazoea kwa hali hii yafaa kweli kuwekwa kwenye kundi la jamii ya watu walioelimika na kustaarabika? Unamkamata vipi mtu kama ushahidi haujakamilika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…