Baada ya kukamilika siku 14 za msamaha kwa wahujumu, Je Rais Magufuli atumie busara za Harun El Rashid kuwasamehe ambao hawakuandika barua? Au...!.

S

sweettablet

JF-Expert Member
5,028
2,000
Pasco kwa hili bandiko lako, I beg to differ. Yaani mtu kagoma kukuandika barua siku 14 alizopewa halafu Rais amsamehe tu! Kwangu hapana! Huyu kesi iendelee mpaka hadi aidha mahakama imtie hatiani au imwone hana Hata. Najua kwamba Pasco unajua Hata nchi zingine, ukigomea amnesty kama hii maana yake uko tayari kufuata utaratibu wa kawaida wa kimahakama. Ingawa nasikia ukitiwa hatiani adhabu yake inakuwa kubwa kweli kweli kwasababu ya "Kuisumbua" mahakama.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,669
2,000
Wanabodi,

Zile siku 14 za msamaha wa rais Magufuli za kuandika barua kukiri makosa na kuahidi kutorudia tena na kulipa walichoiba zimekamilika. Ofisi ya DPP imeishaanza kuzifanyika kazi kwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani ili kuisajili misamaha hiyo kimahakama, kwa barua hizi kupokelewa mahakamani kama uthibitisho wa kukiri kutenda kosa, mahakama itatoa hukumu ya kiasi fulani cha faini ya makosa hayo, mtuhumiwa akilipa faini hiyo anaachiliwa na kuendelea kulipa lile deni alilosababisha kidogo kidogo kwa utaratibu watakaokuwa wamekubaliana na DPP. Hivyo watuhumiwa wenye cash cash ya ukweli, kuanza kuanza kuachiliwa anytime from now maana barua hizo zimeanza kuwasilishwa mahakamani siku ya jana.

Hoja ya bandiko hili ni ni kwa wale ambao wana kesi za uhujumu na utakatishaji fedha, lakini hawajaandika barua za kukiri makosa na kuomba msamaha. Jee kutoandika barua huko ni uthibitisho kuwa wamebambikiwa?. Jee tuwaombee msamaha kwa rais Magufuli atumie uadilifu wa Harun El Rashid kuwasamehe?.

Uandilifu wa Harun El Rashid katika kushughulikia mashauri, nimeuzungumza hapa
https://www.jamiiforums.com/threads...u-harun-el-rashid-wa-alfu-lela-ulela.1194175/
Lakini kwa faida ya wale wavivu kufuata links, ninakuwekea hapa kisa kimoja cha Mwanamke Tajiri na Mwanamke Masikini kilichoamuliwa na Harun el Rashid.

Katika wahujumu na watakatishaji fedha, kuna makundi matatu ya watu na aina tatu za wahujumu.
Tukianza na makundi ya wahujumu, kuna wahujumu wakubwa, matajiri wenye uwezo wa kulipa chochote. Kuna wahujumu wa kati ambao ni watu wa kawaida, na wahujumu wadogo, masikini wa kutupwa hata wakiandika barua za msamaha, hawana uwezo wa kulipa chochote.
Tukija makosa ya uhuhujumu ya kuombea msamaha
1. Kuna Wahujumu kweli na watakatishaji kweli pesa, hawa wataomba msamaha na pesa wanazo na watalipa pale pale watakuwa huru.
2. Wahujumu waliohujumu kidogo na kubambikiwa kesi kubwa, hawa pia wataandika barua na kulipa kulipa kidogo kidogo.
3. Waliobambikiwa kesi za uhujumu, kwenye kundi hili la waliobambikiwa, nako kuna makundi matatu yake.
1 Waliobambikiwa lakini ni matajiri, hawa wataandika barua na kukiri uhujumu ili tuu kuununua uhuru wao kwa gharama yoyote, hawa watalipishwa na watalipa ila kwa vile wamelazimika kukubali tuu ili wawe huru, fedha zao zina bad karma ya malipizi, Mungu atawalipia.
2. Kuna waliobambikiwa ni watu wa kawaida na wengine ni masikini, hawa pia wangetamani kuandika barua wakiri watoke na wengine watakuwa wameandika barua kukiri kwa kusisitiza kuwa wamesingiziwa, ili watoke, lakini pia watakiri kuwa wangekuwa na fedha pia wangelipa, hawa pia wanapaswa kuachiwa bila kulipa chochote.
3. Kundi la tatu, hawa ni watu wakweli, ambao wataamua kusimama na ukweli mpaka mwisho kuwa wao wamesingiziwa, sio wahujumu, hawataandika barua za kukiri makosa ya kubambikiwa, au wakiandika sio kukiri bali kusisitiza wamesingiziwa, hawa ndio Mungu atasiimama nao.

Sasa kwa kuutumia uadilifu na busara kama za Khalifa Harun el Rashid, jee tumuombe rais Magufuli atumie huruma yake na busara zake kuwasamehe kwa kumuelekeza DPP (japo DPP hatakiwi kuelekezwa, siku hizi DPP anaelekezeka!), kutumia powers zake za Nolle kwa kuwatendea haki watu hawa waliobambikiwa kesi za uhujumu kwa kuzifuta kesi zao?.

Kama nilivyo sisitiza wakati wa kumpongeza rais Magufuli kwa uamuzi huu, naendelea kusisitiza rais Magufuli akitenda haki, yeye atabarikiwa na taifa litabarikiwa. Hawa watu waliobambikiwa kesi za uhujumu wakati kiukweli kabisa sio wahujumu, nao watendewe haki.

Hivyo tumuombe rais Magufuli, aombe kupewa majina ya wahusika wote wa kesi zote za uhujumu aangalie ni wangapi hawaja andika barua za kukiri na kuomba msamaha?, then hao wote ambao hawajaandika barua, ndio watakuwa wamebambikiwa, ili ikimpendeza, ndipo amuelekeze DPP, hao wote waachiwe kwa Nolle, watakuwa ni kweli wamesingiziwa na wakiachiwa watakuwa wametendewa haki.
Mungu mbariki rais Magufuli,
Mungu ibariki Tanzania.
Paskali
Ndugu Mayalla ungekuwa kweli uko objective na mwandishi ambaye yuko impartial ungekuwa pia unaandika kukemea kauli na matendo yanayotoka upande wa watawala. Unatumia taaluma yako kwa maslahi yako binafsi. Katika mazingira ya sasa kukaa kimya ni bora zaidi kuliko na utaonekana impartial kuliko kuendelea kutoaka maandiko ambayo biased huku ukitengeneza njia ya malengo yako binafsi. Uwe na siki njema.
Mdomo Mwepesi, karibu, shuhudia jinsi ninavyosifu
P.
 
B

BIGGAG

JF-Expert Member
224
500
Naomba link ya hilo bandiko, umri wa mtoto Kitanzania kwa maana ya minor ni under 14, the age of majority kwa Tanzania ni 18 years. Hao wanaoitwa watoto ni watu wazima wamemaliza vyuo vikuu, wanakaa makwao na wana maisha yao, they are adults na wako responsible kwa maisha yao.
P
Huna haja ya kumjibu, mada iliomezani inaeleweka, achana na destructors.
Na Kama kuna concern apeleke jukwaa husika.
 

Forum statistics


Threads
1,424,956

Messages
35,077,075

Members
538,169
Top Bottom