Baada ya kufanyiwa CT-Scan ya tumbo, hali imebadilika na kuwa mbaya

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
726
564
Wanajf ni siku ya tatu leo toka nifanyiwe ct scan ya tumbo. Ajabu tumbo sasa limebadilika. Linawaka moto.Kiuno sasa kinauma sana. Tumbo linaunguruma sana utafikiri vyura vinafanya mazoezi.

Kelele zinasikika hadi nje ya tumbo. Mgongo una maumivu mpaka leo.Kichwa ndiyo usiseme. Sasa nimekuwa mchovu mno kiasi cha kushindwa kufanya hata yale masuala yetu ya usiku ya baba na mama. Jamani nisaidieni tatizo ni kipimo au ni maradhi yanayonisumbua ambayo bado sijayagundua?

Msaada tafadhari
 
Wanajf ni siku ya tatu leo toka nifanyiwe CT SCAN YA TUMBO.AJABU TUMBO SASA LIMEBADILIKA.LINAWAKA MOTO.KIUNO SASA KINAUMA SANA.TUMBO LINAUNGURUMA SANA UTAFIKIRI VYURA VINAFANYA MAZOEZI.KELELE ZINASIKIKA HADI NJE YA TUMBO.MGONGO UNA MAUMIVU MPAKA LEO.KICHWA NDIYO USISEME.SASA NIMEKUWA MCHOVU MNO KIASI CHA KUSHINDWA KUFANYA HATA YALE MASUALA YETU YA USIKU YA BABA NA MAMA.JAMANI NISAIDIENI TATIZO NI KIPIMO AU NI MARADHI YANAYONISUMBUA AMBAYO BADO SIJAYAGUNDUA?MSAADA TAFADHARI
Kwani unasumbuliwa na nini mpaka ukafanyiwa CT scan?
 
Kwani unasumbuliwa na nini mpaka ukafanyiwa CT scan?
Tumbo linanisumbua sana huu mwaka wa 13.Nimetibiwa sana iwe tiba mbadala au tiba hizi za kisasa.

Daktari huyu mpya ndiyo kadai nifanyiwe CT SCAN TUONE KAMA TUMBO LIKO SALAMA AU LILISHAOZA.

Maana hata haja ninazotoa zina harufu kali sana ningekuwa naweza kuipaste hapa hiyo harufu ningeweka ili mnisaidie.Kiufupi tatizo ni tumbo!!!!!
 
Vidonda vya tumbo huna?
Yaani ni ajabu,vipimo vyote nilivyofanyiwa yaani Barium meal,Barium enema na CT Scan hakuna ambacho kilishaonyesha kuwa nina ugonjwa.

Wale wa tiba lishe ndiyo walidai eti baada ya kunipima nina vidonda.Wakaanza kunitibu hali ndiyo ikawa mbaya mara 10.

Yaani wale ndiyo siwezi hata kumshauri mtu awaone,wengi ni waongo na wako tu kutafuta pesa. Mpaka sasa hapa ninapoongea hali ni mbaya tumboni, kama nilivyoeleza.
 
Tafuta dawa ya asili inaitwa Aswat, ila utaharisha sana ila baada ya hapo unapona kabisa. Nenda kwenye misikiti humo wanzo dawa hizo afu utaleta mrejesho hapa. Ila ukiziendekeza hizo hospitali ujue unakitafuta kifo mapema sana.
Asante kwa ushauri,nimeshapewa dawa za kuharisha za aina mbili.LAKINI WAPI.NILIISHIA KULALA CHOONI NIKIHARISHA NA BASI.UNAFUU HAKUNA!!!HATA HAPA NINAYO MOJA INAYOFUATIA
 
Yaani ni ajabu,vipimo vyote nilivyofanyiwa yaani Barium meal,Barium enema na CT Scan hakuna ambacho kilishaonyesha kuwa nina ugonjwa.Wale wa tiba lishe ndiyo walidai eti baada ya kunipima nina vidonda.Wakaanza kunitibu hali ndiyo ikawa mbaya mara 10.Yaani wale ndiyo siwezi hata kumshauri mtu awaone,wengi ni waongo na wako tu kutafuta pesa.Mpaka sasa hapa ninapoongea hali ni mbaya tumboni,kama nilivyoeleza.
Je kipimo cha endoscopy kile cha kuingizwa mpira tumboni umeshafanya?
 
Je kipimo cha endoscopy kile cha kuingizwa mpira tumboni umeshafanya?
Naomba unieleweshe hicho kipimo kinakuwaje maana nimeshafanyiwa vingi mpaka ninavichanganya!Ila kuna kuna kipimo ninakumbuka dawa ilichanganywa na maji.Ikawekwa kwenye tubes fulani ikaingizwa tumboni mwangu kupitia haja kubwa picha ikachukuliwa.
 
Mioz ya ct scan sio mizur na inashauriwa usifanyiwe Mara kwa Mara at least once per year unless ni lazma
 
Kamuone daktari. Huku utaingizwa chaka tu.
Mpaka hapa nina attend medical clinic ya hapa rufaa Mbeya.Cha ajabu ni kwa kuwa hadi leo siujui ugonjwa unaonisumbua.

Madaktari wenyewe huwa wanaitana na kujadili hali yangu huishia kubishana tu.Hali ninayoexperience sasa hivi ni kuwa daktari wa leo unamkuta anatofautiana na aliyemtangulia.

Hapa nilipo nimeandikiwa dozi za dawa nikipima hivi vidonge kwenye mzani vinakarikia robo tatu ya kilo!!!
 
Yaani ni ajabu,vipimo vyote nilivyofanyiwa yaani Barium meal,Barium enema na CT Scan hakuna ambacho kilishaonyesha kuwa nina ugonjwa.Wale wa tiba lishe ndiyo walidai eti baada ya kunipima nina vidonda.Wakaanza kunitibu hali ndiyo ikawa mbaya mara 10.Yaani wale ndiyo siwezi hata kumshauri mtu awaone,wengi ni waongo na wako tu kutafuta pesa.Mpaka sasa hapa ninapoongea hali ni mbaya tumboni,kama nilivyoeleza.
Pole sana... Nenda Nairobi ukirud utakua umepona kabsa na unilete na zawad ya earphone
 
Pole sana Mkuu!
Inawezekana madaktari hawazungumzi vizuri na wewe, na pia inawezekana wewe mwenyewe hudadisi shida yako. Tiba siku hizi ni lazima ujadiliane na daktari. Na hata akikupa dawa fulani ni lazima muongee kazi za hiyo dawa, madhara yake n.k.

Umekutana na specialist au daktari wa degree moja au unakutana na vishoka?

Hao Mbeya Rufaa wameshanunua CT scan? Nakumbuka mara ya mwisho Kigwa aliwaambia wanunue.

Ni PM kuna vijana wazuri nawafahamu kule.

Mpaka hapa nina attend medical clinic ya hapa rufaa Mbeya.Cha ajabu ni kwa kuwa hadi leo siujui ugonjwa unaonisumbua.Madaktari wenyewe huwa wanaitana na kujadili hali yangu huishia kubishana tu.Hali ninayoexperience sasa hivi ni kuwa daktari wa leo unamkuta anatofautiana na aliyemtangulia.Hapa nilipo nimeandikiwa dozi za dawa nikipima hivi vidonge kwenye mzani vinakarikia robo tatu ya kilo!!!
 
Yaani ni ajabu,vipimo vyote nilivyofanyiwa yaani Barium meal,Barium enema na CT Scan hakuna ambacho kilishaonyesha kuwa nina ugonjwa.Wale wa tiba lishe ndiyo walidai eti baada ya kunipima nina vidonda.Wakaanza kunitibu hali ndiyo ikawa mbaya mara 10.Yaani wale ndiyo siwezi hata kumshauri mtu awaone,wengi ni waongo na wako tu kutafuta pesa.Mpaka sasa hapa ninapoongea hali ni mbaya tumboni,kama nilivyoeleza.
Cheki na mashehe, litakuwa jini hilo, likitolewa waponaa, usihofu hujachelewa, utapona tuu (shehe msopa majini - mabibo)
 
Ila pamoja na hayo bado hujatoa maelezo yako vizuri ya maumivu ya tumbo ndo maana labda hupati matibabu sahihi.

Unaumwa tumbo lipi sehemu ya juu au chini au lote? Je choo chako kikoje? kama umeangaliwa na ct scan na hawajaona hata cancer(tumor) Basi inawezekana ni life style yako mbovu, ningefahamu pia physiology yako ulivyo na namna unavyokula na kunywa, na huwa tumbo lako linauma wakati gani au muda wote...ili usaidiwe lazima diagnosis ya kutosha ifanyike.

Ila nakushauri tu epuka sana dawa za hospitali kabla hujajua unaumwa nini yawezekana hizo dawa ndo zikakupa ugonjwa zaidi. na pia umri wako ungefahamika pia...
 
Back
Top Bottom