Narudia tena kusema kwamba kama unaongelea Askofu Zakary Kakobe kukutwa na anguko kama hilo(kuzini) mtasubiri sana. Si kwamba yeye ni malaika lakini kwa maombi tunayomwombea usiku na mchana haitokaa itokee. Nakuhakikishia.
Kazi yetu ni kuwaombea watumishi wa Mungu kwamba awalinde na yule mwovu asiwaweze, maana shetani hapendi kuona kazi ya Mungu ikiendelea. Kimsingi kila muumini anapaswa kumwombea Mchungaji wake anayemchunga kiroho, wengine wanaangushwa na dhambi kama hizo za uzinzi kwasababu waumini hawasimami katika zamu zao kuwaombea kwa uchungu na bidii.
Kunatofauti kubwa kati ya kumwombea na kumtumaini mtu. Sisi tunamwombea ili Mungu azidi kumlinda. Mungu ndiye tunaye mtumaini peke yake kwakuwa tunajua anayemtumaini mwanadamu amelaaniwa.
Nyaya za umeme pale makao makuu zilizopitishwa kwa nguvu na Tanesco haziwaki mpaka hivi sasa tunavyoongea.