Baada ya Ajali ya Kivuko Kilombero,Sasa Wananchi wavusha magari kwa mtumbwi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865

Baada ya ajali ya Kivuko kutokea katika mto Kilombero,sasa wananchi wenye "ujuzi" wa kupalaza wanatumia mitumbwi kuvusha magari toka upande mmoja kwenda mwingine.Mitumbwi hiyo inaonekana kuwa duni na kuweza kusababisha usalama wa magari,watu na mali zao.
Kwa kuzama Kivuko hicho,sasa safari za kuvuka toka Kilombero kwenda Upande wa pili zimekuwa ngumu na zisizo salama kabisa

MITUMBWI YAVUSHA MAGARI

Baadhi ya Wananchi waishio na kufanya biashara za Madini wilayani Ulanga mkoani Morogoro wanavusha Magari yao madogo kwa kutumia Mitumbwi katika Mto Kilombero kwa kutokea upande wa Kilombero kwenda upande wa Mahenge, Ulanga.

Kuzama kwa Kivuko cha MV Kilombero 2 mwishoni mwa mwezi wa kwanza mwaka huu katika mto Kilombero kumesababisha baadhi ya Wafanyabiashara kuvusha Magari yao kwa kutumia Mitumbwi ili hali ni hatari kwa maeneo hayo ya Mto ambao hujaa maji kila mara.
Source:Azam News Online
 
Back
Top Bottom