Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,422
- 5,026
Kuanza biashara ni jambo moja lakini kuiendesha isimame na kudumu ni jambo lingine tena linalohitaji kutuliza akili na kuwa na nidhamu sana katika biashara.
Zipo biashara ambazo huanzishwa na hatimae hufa kwa sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo ni kama zifuatazo:-
Mazingira/wakati kutokua rafiki na bidhaa yako. Huenda uchaguzi wa eneo la biashara hukulifanyia utafiti wa kutosha kabla ya kuanzisha aina hiyo ya biashara na hivyo baada ya kufungua ukakuta bidhaa unayouza haihitajiki sana eneo hilo au muda huo.
Ushindani wa kibiashara.Inawezekana kuna mtu kafungua biashara kama yako na hivyo kakuzidi kiushindani na kuchukua waliokuwa wateja wako na hivyo kupelekea mauzo yako kushuka na biashara kuelekea kufa kabisa.
Ubovu wa huduma kwa wateja. Inawezekana ulipofungua biashara ulipata wateja lakini baada ya kipindi Fulani wateja wakakukimbia kutoka na utoaji wako huduma, ni kwa vipi unawasiliana na wateja wako. Je, wanafurahia lugha yako na huduma yako au wanakwazika?
Majanga. Kuna majanga yanaweza tokea yakapelekea biashara kuzorota kabisa mfano kwa sasa kuna corona.
Kukosekana kwa hela kirahisi(Mikopo) Kuna wakati biashara inataka kupewa nguvu hela ikikosekana inashindwa kustawi.
Uongozi. Iwapo umemwajiri mfanyakazi katika biashara yako unamuongoza vipi? Ukimfanya ajione anatengwa na sio sehemu ya biashara ni rahisi kufanya uzembe na kukuingiza hasara kwenye biashara.
Hivyo basi ukiona biashara yako inashuka au inakaribia kufa fanya utafiti ili kujua ni kitu gani kinasababisha na uchukue hatua madhubuti.