Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Wakazi wa vijiji vya Sepisa na Hombolo katika Kata ya Hombolo mkoani Dodoma, wamekuwa wakishindia uji wa ubuyu kutokana na ukosefu wa chakula, huku bei ya unga wa sembe ikiwa juu tofauti na siku zote.
Kutokana na hali hiyo, wameiomba Serikali iwapatie msaada wa chakula kutokana na njaa inayoikabili kata hiyo.
Pia wamesema ndege waharibifu wa mazao, kwelea kwelea, wamevamia mtama katika baadhi ya vijiji vya kata hiyo na kusababisha hofu kubwa kwa wakulima wanaotegemea zao hilo kwa chakula.
Wakizungumza na waandishi wa habari juzi, wakazi hao walisema upatikanaji wa chakula katika kata hiyo si mzuri kwa vile kilo moja ya unga hivi sasa inauzwa kwa Sh 2,500 bei ambayo ni kubwa ikilinganishwa na uwezo wa wananchi wengi ambao ni masikini.
Nizar Wanjali alisema kutokana na tatizo la njaa familia nyingine zimekuwa zikishindia uji wa ubuyu baada ya bei ya mahindi kuwa juu.
“Hali ni mbaya, familia nyingine zinashindia uji uliotengenezwa kwa unga wa ubuyu,” alisema. Alisema biashara iliyopo sasa ni ya ubuyu, ambao debe moja limekuwa likiuzwa kwa Sh 1,000.
“Watu wanauza ubuyu wakipata fedha ndiyo waweze kununua unga,” alisema.
Naye Raphael Masima alisema debe moja la mahindi limekuwa likiuzwa kwa Sh 25,000 hali ambayo inafanya wananchi wengi washindwe kumudu na kujikuta wakila mlo mmoja kwa siku.
Neema Matonya alisema uhaba huo wa chakula umesababisha wafugaji wa nguruwe kuacha kufuga kutokana na kupanda bei ya pumba ambako debe moja kwa sasa linauzwa kwa Sh. 4,000.
Alisema hali hiyo imesababisha watu kuacha kufuga na hata nguruwe waliopo wamedhoofu kwa uhaba wa chakula. Diwani wa Viti Maalum, Editha Luhamo (CCM) amekiri kuwapo tatizo la njaa huku akidai kuwa mtama ambao ulianza kuchanua umeanza kuliwa na kwelea kwelea.
“Sasa ninafanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya kilimo waweze kutusaidia katika tatizo hili,” alisema. Pia alisema hali ya mazao katika kata hiyo ni mbaya kutokana na mazao kuanza kukauka kwa jua kali.