Baa la njaa:Ushauri Kwa mheshimiwa Rais

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,655
Najua mheshimiwa Rais si mtu anayependa kushauliwa hasa na watu anaohisi hawakumuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka jana.

Natambua kua hata kauli zake za kero na kebehi kwa wananchi wake zinatokana na ukweli anaoujua juu ya ushindi wake kama ulitokana na wingi wa kura harali au za ukokotoaji.

Cha msingi, kama ambavyo amekuwa akisisitiza kila mara kwa namna ambayo kimsingi ni ya kumjenga yeye mwemyewe kisaikolojia, Kwamba yeye ndio Rais. Na mimi nakubaliana nae yeye ndio Rais wetu.

Hivyo nachukua fursa hii, hasa kutokana na kuamini mheshimiwa Rais ni mpenzi wa Mungu kumshauri atafakari upya juu ya msimamo wake juu ya baa la njaa linalosemwa sana kila kukicha siku za karibuni hasa na yeye.

Natambua msimamo wake umejikita zaidi Kwenye misingi miwili
1.Biblia inasema asiyefanya kazi na asile
2.swala la chakula sio jukumu la serikali.

Namshauri akasome Biblia yake tena,katika kitabu cha Mwanzo kumeandikwa habari ndefu sana juu ya baa la njaa liliukumba ufalme wa farao huko Misti.

Imeandikwa namna farao mfalme, Kama alivyo yeye mheshimiwa magufuri Leo kwa taifa letu,hatua alizochukua kukabiliana na tatizo hilo ikiwamo kuufumua na kutengeneza muundo mpya kabisa wa kiutawala aliiusimika juu ya kijana ambae achilia mbali hakuwa raia wa taifa hilo bali alikuwa mfungwa kwa kosa linalohusisha udharirishaji mkubwa kwa Farao mwenyewe na taifa zima.

Najua msingi mkuu wa utawala wako ni chuki, hivyo naamini ukipitia habari hiyo kwa utulivu na ukamuuliza Mungu kama kuna hatua za kuchukua Nyongo yote ya chuki inayokutafuna itakutoka na kama kweli kuna baa la njaa basi utaweza kutuvusha wananchi wako kwenye janga hili salama.

Zaidi nakuombea Roho ya unyenyekevu na busara za uongozi namuomba Mungu akubariki Katika hayo mawili japo kidoooogo.
 
Back
Top Bottom