Azimio la arusha (ndoto yangu ya kusadikika)

Azimio la arusha (ndoto yangu ya kusadikika)

Denge Boy

Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
6
Reaction score
1
Ndoto yangu ya kusadikika imekuwa inanisumbua kwa kiasi kikubwa sana na kusababisha nipachikwe majina mengi likiwamo la "The day Dreamer".

NINGEPENDA JAPO KWA KIFUPI NIJARIBU KUWASHIRIKISHA WANA JAMII FORUMS katika mojawapo ya NDOTO ZANGU ZA MCHANA Kuhusu AZIMIO LA ARUSHA.
IFUATAYO NI NDOTO YANGU YA KUSADIKIKA:-
Unapocheza ngoma ya Kimakonde iliyobuniwa na Wamakonde na kuwekewa sheria za uchezaji na mmakonde, ni dhairi kuwa itakupasa kufuata vigezo na masharti ya ngoma hiyo kama vilivyowekwa na mmakonde.
Kwa Mtazamo wangu napenda kusema kuwa, Hayati Baba wa Taifa pamoja na Think Tankers wenzake walipoliasisi Azimio la Arusha, Mataifa Makubwa (Yaani wale wakoloni ambao safari hii waliamua kuishi chini ya kivuli cha Ukoloni Momboleo) waligundua ya kuwa, Azimio la Arusha ni Ngoma mpya ya Kitanzania, iliyobuniwa na waasisi wa Taifa letu la Tanzania kwa manufaa na Maendeleo ya Taifa letu, na pia ilikuwa ni Nzuri sana na inauwezo wa kumtoa Mtanzania katika makucha ya Ukoloni Momboleo na kumfikisha katika kilele cha mafanikio.
Na kwa kuzingatia mtazamo wangu kuwa Ukoloni Momboleo ulikuwa umejikita hasa kwenye Matumizi ya Akili kwa kiasi kikubwa sana (Upeo mkubwa wa Ki-Intelijensia) sambamba na matumizi ya nguvu kidogo (hapa kuna kitu ambacho siwezi kukithibitisha lakini kinafahamika kama Possible Denial Events), tutaona kuwa Mkoloni asingeweza kukubali kuona anaachilia mbali utajiri wote uliopo katika Ardhi ya Tanzania, na hapa ndipo ndoto ya kusadikika inapoanzia.
Kwakuwa mfumo wa ukoloni Momboleo ni Matumizi ya Intelijensia ya hali ya juu na utekelezaji wa matukio yanayofahamika kitaalamu kama possible denial events basi ni dhahiri kulikuwa na umuhimu wa kulivunja Azimio la Arusha kwa namna ambayo mtu yeyote asingethubutu kuwatuhumu Wakoloni kuhusika na Hujuma hiyo. Pengine hapo ndipo mipango ya kuyumbisha uchumi wa Taifa na kuitafutia sababu Tanzania kujiunga na IMF pamoja na World Bank ili kuifanya Tanzania iendelee kucheza ngoma ya Kikoloni Chini ya Masharti ya "Binafsisha mashirika ya umma, punguza ukubwa wa ajira serikalini, vunja vitengo fulani vya serikali au viunganishe." Kama Mwana Jf HighLander alivyoelezea.
Hapa naweza kusema kuwa kumchochea Idi Amini Kupigana na Tanzania Isingeweza kuwa kazi ngumu kwani inafahamika kuwa Amin hakuwa mtu mwenye uwezo wa kusoma Ishara za Nyakati vizuri, hivyo hata wafadhili wake kina Gadaffi wangeweza kumshawishi kirahisi chini ya influence ya wakoloni japo Wakoloni wenyewe walichotaka ni kuiingiza Tanzania katika vita, na kuifilisi kiuchumi ili iweze kuona umuhimu wa kujiunga na IMF na WORLD BANK. Hapa ikumbukwe kuwa baadhi ya wachambuzi wa mambo walikwenda mbali na kusisitiza kuwa Hayati Baba wa Taifa hakuwa tayari kujiingiza katika vita kwa kuhofia kuyumba kwa uchumi mpaka pale Mwae ambaye alikuwa ni rubani wa ndege za kivita alipoduguliwa na Idi Amini (That was a way of provoking him kama sijakosea).
Yaliyofuata baada ya vita kuisha na Tanzania Kutetereka kiuchumi tunaona kuwa ni yaleyale yaliyopangwa, yaani Tanzania kujiunga katika Ngoma ya Wakoloni na ambayo matunda yake ni mizizi ya rushwa ambayo ilishamiri na kuzaa Azimio la Zanzibar.
Zaidi ya hapo tunaona kuwa walewale(wakoloni) waliofanikisha kuizuia Tanzania isiendelee na ngoma ya Kitanzania (Azimio la Arusha), sasa wanafadhili Chama Fulani cha siasa na kukifundisha namna ya kufanya propaganda zisizo na nia nzuri huku mabosi wao (wafadhili wao) wakiwatumia Secret Operatives wao Kukamata baadhi ya Watanzania na kuwanyofoa kucha na meno (Waandishi wa Habari, Madaktari) na baada ya kutekeleza hayo, watumwa wao (Chama fulani cha siasa) ambao pia naweza kuwaita wasaliti kwa Taifa letu, wanaongozwa kuzidi kufanya propaganda na kuwahimiza Watanzania kufanya migomo ya kila namna na kusababisha Watanzania wenyewe kwa wenyewe tuanze kushikana uchawi bila kuelewa kuwa bado Tunachezeshwa ngoma ya mkoloni ambayo inaongozwa na wasaliti Fulani (vibaraka) ambao matarajio yao ni misaada wanayozania kuwa itawasaidia kuingia ikulu pasipokujua kuwa hata kama wangebahatika kuingia Ikulu, bado wasingekuwa na sauti juu ya uongozi wa Taifa hili hasa kwakuwa wao ni vibaraka tu na watabakia kuwa vibaraka tu.
Kwa kifupi, hii ni ndoto yangu ya kusadikika. Kama kawaida natarajia vipofu wa akili na fikra hawataipita thread hii au la kutoa matusi na kejeli, lakini wenye upeo wataichungulia na kutoa comments as think tankers do.
 
Back
Top Bottom