Azerbaijan:Hatujairuhusu israel kutumia ardhi yetu au anga kuishambulia iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
AZERBAIJAN YAFYATA MKIA KWA IRAN.

Balozi wa Azerbaijan Mukhutar Muhammadov amekataa katakata kuhusiana na taarifa za nchi yake kuipa Israel ardhi yake kuishambulia Iran.

Balozi huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa anafanya mahojiano na mwandishi wa habari wa The Jerusalem Post / JPost.com huku akisisitiza kwa kusema, kamwe Azerbaijan haiwezi ikaipa kambi Israel kuishambulia Iran wala kuruhusu ndege za kivita za Israel kujaza mafuta nchini Azerbaijan.
 
Western wanaona halali kwa Israel kuishambulia Iran lakini sio halali kwa Russia kuiahambulia Ukraine

Nikirudi kwenye topic, Israeli hawezi hata kijaribu kuishambulia Iran., ataishia ktk kuchimba mikwala mbuzi tu
 
Cha kushangaza sijui ilikuwaje wanasayansi kadhaa wa Kiiran huuawa ndani ya nchi yao anasingiziwa Israel
Kumuuwa mtu haimaanishi kufanya direct war haitatokea abadani Israel mwenyewe anajua kitakachotokea ni kichaa tu ndyo anaweza Fanya ivyo kwa kisingizo cha nyuklia ila madhara yake ni makubwa kuliko Irani kumiliki nyuklia
 
Western wanaona halali kwa Israel kuishambulia Iran lakini sio halali kwa Russia kuiahambulia Ukraine

Nikirudi kwenye topic, Israeli hawezi hata kijaribu kuishambulia Iran., ataishia ktk kuchimba mikwala mbuzi tu
Kemea uvamiz wa aina yoyote sio mpaka West waanze kulalamika
 
Cha kushangaza sijui ilikuwaje wanasayansi kadhaa wa Kiiran huuawa ndani ya nchi yao anasingiziwa Israel
Ni kweli anatekeleza hayo anakuwa Israel ila kwenye mwamvuli wa kigaidi, Israel anautaka Usuper Power wa mashariki ha kati japo tishio analolipna ni kwa muiran maana Iran ni Taifa ambalo liko vizur kitechnology hivo hawataki kuwaona Iran wakiwa na siraha za maangamizi! Wanataka Iran iliyo dhaifu na hii inatokana na misimamo ya serikali ya Iran.

Kila Juhud zimefanyika kuingangusha serikali ya Iran lakini mambo yameshindika na ndipo juzi waziri wa Ulinzi wa US anasema kamwe hatarohusu Iran kuwa na siraha za nyuklia! Kwaiyo kwasasa uenda ni kweli wanaandaa mkakati mkubwa wakuitumbukiza Iran kwenye vita
 
Back
Top Bottom