Azam Yapata Pigo Kuelekea Mechi ya Marudiano CAF

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
BEKI wa kati wa Azam FC, Serge Wawa Pascal na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche, wote raia wa Ivory Coast hawatasafiri na timu kwenda Tunisia kesho.
Wawili hao wote watakosekana kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance Jumatano mjini Tunis kutokana na kuwa majeruhi.
Daktari Msaidizi wa Azam FC, Talib Omar ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba Wawa aliumia misuli katika mechi ya kwanza dhidi ya Esperance Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Azam ikishinda 2-1.

Kipre Tchetche hatasafiri na timu kwenda Tunisia kesho kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli

Dk. Omar amesema jithada za kumrejesha mapema uwanjani Wawa zimeshindikana na sasa ataendelea na matibabu na hatasafiri na timu kwenda Tunisia.
Dk. Omar amesema kwamba Kipre naye aliumia Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Azam ikishinda 1-0.
“Kipre naye ameumia misuli pia, kwa hiyo wachezaji hao pamoja na beki wetu mwingine tegemeo, Shomary (Kapombe) ambaye ni mgonjwa wote watakosekana katika mchezo huo,”amesema Dk. Omar.
Lakini Dk. Omar amesema kwamba habari njema ni kwamba kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekuwa majeruhi hadi akaukosa mchezo wa kwanza na Esperance amepona na anatarajiwa kusafiri na timu.
Azam inaondoka kesho kwenda Tunisia ikihitaji kuulinda ushindi wake wa 2-1 nyumbani ili kuingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
 
Ngoja nijiandae kuipenda Azam ili baadae niwe mshabiki wa kudumu wa hiyo club maana naona wana vision sio club yangu Simba ambayo kila mwaka wanatutesa sisi mashabiki kuomba kuiombea mabaya mahasimu wetu hasa match za mwisho ili tuweze kupenya hata shirikisho.Mwaka jana tulikuwa tunaiombea mabaya Azam ila Yanga ikabana match ya mwisho na Azam.Mwaka huu tunaweza kuwa Second runner ila haisaidii tena maana kuna FA na kule tumetolewa.Ngoja nione kama hivi kubadili ushabiki kunawezekana,maana ikiwezekana Simba siishabikii tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom