Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
KITENDO cha Azam kutoka sare ya mabao 2-2 na JKT Ruvu Stars kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam leo kimeipa rasmi Yanga ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2016 kwani sasa vijana hao wa Jangwani wanahitaji pointi moja tu.
Azam ndiyo timu pekee ambayo ilikuwa inaweza kufikisha pointi 71 na kutishia ubingwa wa Yanga, lakini sasa hata kama itashinda mechi zake tatu zilizosalia, itafikisha pointi 69 tu, ambazo kwa zinaweza kufikiwa na Yanga hata kama itatoka sare na Mbeya City Jumanne, Mei 10 jijini Mbeya.
Soma zaidi hapa => Azam waipa Yanga ubingwa Ligi Kuu 2015/2016 | Fikra Pevu