Azam TV wababaishaji

ngulyavyangu

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2019
Posts
203
Reaction score
266
Sijui tuseme ushamba au kukosa ubunifu au ni umaskini tu.
Hawa azam tv Wana App yao, cha kushangaza siku ya mechi wanaizima baada ya mechi wanairudisha.

Sasa najiuliza Hii App wameiweka ili iweje,? Kwa mtazamo wangu Sio lazma uwe na TV unaweza kuwa kwenye daladala ukafungua App unaangalia unachotaka.

Sasa siku ya mechi wanazima App ili iweje [emoji848]
Au watu tubebe Ma TV kwenye daladala.

Hii nchi
 
Basi nikajua ni mimi pekee,kumbe ndivyo walivyo,mpaka mida hii hamna kitu
 
Kwa sababu ni bure, unawapunja wale wanaolipia.
App ya DSTV ipo na huwezi ku_access channel yoyote mpaka uwe na smart card number ya kisimbusi kilicholipiwa na utaangalia za kifurushi husika tu.
Azam nao watakuja huko
 
Soka tunalipenda ila ndo hivyo hatuna morali wowote wa kuhamasisha, li tv la taifa lina channel mbili ila inashindwa kuonyesha hata hii mechi ya kirafiki tukaona timu yetu inaendeleaje sasa hivi wanaonyesha madude ambayo naamini wanaangalia wenyewe studio, ovyo kabisaa, kazi kufanya press conference na kunadi mijezi isiyo na kiwango na kuongea pumba tupu ili kupata political mileage, pumbaavu kabisa wote wanaojifanya kuhamasisha wakati wanashindwa hata kuonyesha ka mechi ka kirafiki
 
wamebadilisha system mkuu...sasahivi unajisajili kwenye app..then kuna premium na free TV..unalipia hamna cha bure..
 
Niliona tangazo la utv kurejea hewani, sijaelewa. Wanarejea kwenye appbyao au luningan? Tusaidiwe hapa
 
Mkuu umeongea point kiukweli TBC bado sana na sasa basi ukiangaria hiyo TBC safari ndio akuna jambo kabisa awana ubunifu vipindi vinajirudia rudia ushauri kama vilaza waende nat geo wild wakajifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…