Azam Media Ltd is coming soon

Azam Media Ltd is coming soon

Trust mi itakuwa TBCCM II cz jamaa ni muoga sana kwa kuhofia biashara zake kupigwa dafrau. Lazima habari zake zinasupport sana CCM hazitakuwa balanced hata kidogo. Bora alete Azam Beer tuendelee kulewa tu. Kwa biashara ya habari atatuchefua 2

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama hataajiri wahindi apewe kibali .. Kama ajira watapewa watanzania hakuna haja ya kumnyima
 
Na ile ishu ya mabasi iliishia wapi?

Atakuwa alipigwa "Biti" na kina Riziwani, kwani nao walikuwa wanalichungulia hilo dili la Public Transport, ndio maana wakaanza kwa kuimaliza UDA....
 
wamiliki wa klabu tajiri ya Azam FC ipo mbioni kumwaga zaidi ya sh. 1.5 bilioni kwa timu zote za Ligi Kuu Bara msimu ujao na itarusha laivu mechi zao kupitia televisheni yao.

Lakini habari za ndani zinadai Simba na Yanga zinagoma zikitaka kuongezewa fungu kwa madai kwamba televisheni ya kulipia itakayoanzishwa na Azam itanufaika zaidi.

Azam imekusudia kuchukua tenda ya kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu Bara kupitia kituo chake kipya cha televisheni (Azam TV) ambacho kitaanza kazi hivi karibuni na ujenzi wa mitambo hiyo unaendelea katika jengo moja lililopo Barabara ya Mandela, jijini Dar es Salaam.

Habari za uhakika zinasema Azam itauza ving’amuzi na inakusudia kutoa kiasi cha Sh. 100 milioni kwa kila timu kwa timu zote 14 zitakazoshiriki ligi msimu ujao.

Jumatano wiki hii Kamati ya Ligi chini ya Wallace Karia na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walikutana na klabu za Ligi Kuu kujadili mkataba huo ambao utazipunguzia mzigo klabu ndogo ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ukata kutokana na kutegemea udhamini wa Vodacom pekee.

Karia alisema: “Tulikuwa na kikao na kuna televisheni moja ambayo tunataka kuingia nayo mkataba.”

Habari za ndani zinasema Azam TV wataingia mkataba wa miaka mitano kuanzia Agosti na itakuwa ikirusha pia ligi za nchi nyingine za Afrika kama inavyofanya Supersport ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, uliibuka mzozo baada ya Simba na Yanga kutaka kupewa mgao mkubwa tofauti na klabu nyingine. Lakini hatma itajulikana wiki ijayo baada ya klabu hizo kukutana tena kujadili mkataba huo, ule wa Supersport pamoja na Vodacom.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alisema; “Hata Manchester United udhamini wake wa Ligi haulingani na Wigan wala Sunderland, wa Man United upo juu kwa vile ni klabu kubwa, sasa iweje sisi tupate sawa na timu nyingine?

“Pili tunataka kuja na mkakati wa kuhakikisha msimu ujao mechi ambazo tutaenda kuzichezea mikoani tunawaachia mapato yote na wao wakija Dar es Salaam mapato ya huku hayawahusu, na huu ni utaratibu wa kawaida tu unaofanyika hata kwenye nchi nyingine, haiwezekani tunatumia shilingi bilioni 2.3 msimu mzima halafu mapato tunayopata ni kiduchu,”alisisitiza Rage.
 
Navyojua TBL na Hii campuny ya kutengeneza masigara haitapata nafasi ya kurusha matangazo yake.
 
Trust mi itakuwa TBCCM II cz jamaa ni muoga sana kwa kuhofia biashara zake kupigwa dafrau. Lazima habari zake zinasupport sana CCM hazitakuwa balanced hata kidogo. Bora alete Azam Beer tuendelee kulewa tu. Kwa biashara ya habari atatuchefua 2

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Mimi nadhani hafungui kituo cha TV, yeye atakuwa kama DSTV, au TING, au STAR TIMES, content zitazooneshwa SIYO ZAKE!
 
Tajiri wetu sasa kaamua kutumia fursa iliyokuwepo kuingia kwenye media industry ya kuanzia satelite tv yake.mchakato sasahivi anaomba kibali TCRA.

Haya sasa waliukowepo wajipange sana sababu huyu mtu analeta ma exparties hamna mambo yakujuana hapa.

Hamna digitek,continental wala startimes itakayofua dafu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Je, wasiovaa vibarkashia nao wataajiriwa humo?
 
Haendi kisanii huyo amefanya kwanza utafiti hafu ndo kapress order scania sweden mwezi wa 6 mabasi 10 ya mwanzo yataingia tokea south a. baada ya kujengwa. Ajira wahi uwe mkata tiketi ha ha ha!
Kwa hiyo dili la mabasi lipo? Ngoja nikafanye mchakato wa kuwa konda hahahaaah!!
 
Tajiri wetu sasa kaamua kutumia fursa iliyokuwepo kuingia kwenye media industry ya kuanzia satelite tv yake.mchakato sasahivi anaomba kibali TCRA.

Haya sasa waliukowepo wajipange sana sababu huyu mtu analeta ma exparties hamna mambo yakujuana hapa.

Hamna digitek,continental wala startimes itakayofua dafu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Mmmnh Wabongo bwana!
Mbona alikuja na maji ya UHAI, lakini maji ya KILIMANJARO hayajafa? Alikuja na AZAM COLA, lakini PEPSI na COCA COLA hazijafa? Kaja na AZAM FC mbona SIMBA na YANGA hazijafa na zinaendelea tu kugawana kutwaa Ubingwa?
Sisi wenyeji hapa mjini tunajua kinachoendelea kwa miradi ya AZAM, wageni wa hapa mjini ndo mtakuja na kauli za macho juu kama mleta thread hii. Ngoja ije tuone, acha mbwembwe za kitoto.
 
inakuja na full channels,mpira uefa,world cup etc.Dstv soon itabidi wachushe bei.
Mheshimiwa umejuaje hayo mambo ya Mzee wa chapati,au nawe ni mdau wa Mzee wa chapati a.k.a Lambalamba
 
Mimi nadhani hafungui kituo cha TV, yeye atakuwa kama DSTV, au TING, au STAR TIMES, content zitazooneshwa SIYO ZAKE!

mkuu kadai anaingia mkataba na vilabu vyote tanzania that means anaanzisha television sio decoder!
 
dah jamaa kaamua kweli....hii ni revenge kwa mengi baada ya bifu la azam cola.
 
mkuu kadai anaingia mkataba na vilabu vyote tanzania that means anaanzisha television sio decoder!

Duh!...wacha tusubiri tuone yeye atasimama upande gani kisiasa, maana kwa Tanzania chombo cha habari kuwa nutral inakuwa mtihani mgumu. Au na yeye anajiandaa kuelekea 2015...huenda kuna mtu anataka kumweka kwenye kiti ili afanye kama mwenzie RA!
 
Tajiri wetu sasa kaamua kutumia fursa iliyokuwepo kuingia kwenye media industry ya kuanzia satelite tv yake.mchakato sasahivi anaomba kibali TCRA.

Haya sasa waliukowepo wajipange sana sababu huyu mtu analeta ma exparties hamna mambo yakujuana hapa.

Hamna digitek,continental wala startimes itakayofua dafu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
unafikiri hawezi kununuliwa na ccm kama wenzie?????tunaomba ufafanuzi mkuu tujue pia mahusiano yake na CCM, vinginevyo hivi vilivyopo vinatutosha tu kwakweli hatuhitaji maudhi zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom