Ayoub Lakred mnamchukulia poa atawashangaza!

Ndio ninesema mna ujuaji hali yakuwa hata mpira hamujui hivi yale magoli unaweza kumlaumu kipa kwa lipi?

Tuanze na goli alilo fungwa siku ya mechi ya power Dynamos huko zambia, kwanza mshambulia aliye funga hilo goli movement yake aliyo kuwa anaifanya akiwa na mpira haikuonesha dalili yeyote iwapo yule jamaa alikuwa anajiandaa kushut, kwa sababa mbele yake kulikuwa na mabeki zaidi 3 wa Simba walikuwa mbele yake na pia alikuwa mbali sana na goli .Inamaana alifanya maamuzi ya kushut baada ya kuona mabeki wa simba walio kuwa wamenzunguka wanamkaba kwa macho ,kitu ambacho kipa hakukitegemea maana aliamini mabeki walikuwa na uwezo wa kumbrock yule mfungaji wa goli. Alafu kingine lile shuti lilikuwa kali japo lilikuja liambaa ambaa kwa chini alafu ule mpira ulikuwa unandunda ndunda kwa chini , hilo goli badala ya kumlaumu kipa, una takiwa kuwalaumu mabeki kwa kushindwa kutimiza majukumu yao na umsifu mfungaji wa lile goli maana alifanya maamuzi magumu na katika wakati usio tegemewa.

Goli alilo fungwa hapa dar sasa hilo ndo kabisa haitaji hata chembe ya lawama maana mchezaji aliye funga lile goli alitoka na mpira karibia na katikati ya uwanja akamove nao kwa zaidi ya sekunde 45 wachezaji wa simba wanamuangalia tu akasoge mpaka nje kidogo ya box wachezaji wa simba wanamuanalia tu, akasegea mpaka katikati ya mabeki 4 wa simba akashot sasa hapo kipa aunamlaumu kwa lipi zaidi ya kuleta ujuaji usio na maana?

Nyinyi ndo mnamlaumu kipa ya taifa staz kwa kufungwa bao la mbali na Hakim Zieych hali ya kuwa magoli ya aina hiyo amekuwa akiyafunga kwenye mechi nyingi tena dhidi ya magoli kipa bora duniani.
Hata kipindi kakolanya yupo Simba, akipewa nafasi ya kucheza Badoo mashabiki wanalalamika, saivi yupo Singida ndio wanaona Bonge la kipa

Ila huyu kocha si kasema hata angalia jinaa Bali uwezo wa mchezaji tusubiri tuone.

Tatizo hii Simba yetu changamoto kubwa baadhi ya wachezaji wao ni wakubwa kuliko timu, hayo Mambo yashapitwa na wakati, huchezi vizuri benchi mwingine apatiwe nafasi
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Lakred naamini ndiye kipa no 1 Simba sports club
Anayefuatia kwa ubora ni ALLY SALUM

Manula tangu apigwe goli 5 namwona siyo mzalendo kwa timu, Ana tamaa sana
Kuna mdau huko juu alihoji VP LAKRED angedaka ile mechi na mtaani saivi angekuwa wapi?? Ni obviously mizigo yote angebebeshwa yeye hata kina Mangungu sasinge husika
 
Goal alilofungwa onana mechi dhidi ya chelsea angefungwa ayoub maneno yangekuwa mengi sana

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hata magoli aliyo fungwa manura siku ile ya Yanga yalikuwa magoli malaini sana ,sema tu alijificha kwenye kichaka cha ajacheza muda mrefu,sasa sijui angekuwa huyu muarabu sasa hivi nadhani angekuwa amesharudishwa Morocco.
 
Hata magoli aliyo fungwa manura siku ile ya Yanga yalikuwa magoli malaini sana ,sema tu alijificha kwenye kichaka cha ajacheza muda mrefu,sasa sijui angekuwa huyu muarabu sasa hivi nadhani angekuwa amesharudishwa Morocco.
Hata Mangungu, try again vile vikao vyao vya mchongo visingekuwepo
 
Kama uliangalia ile game Vs Asec save aliyofanya aisee Ni bonge la kipaa, binafsi sielewagi kwanini huyu mwamba anapondwa, makosa yapogo tuu kwenye mpira Ni kipa gani duniani mzuri hajawahi kufanya makosa ya kiboya?

Ana footwork nzuri Sanaa na Ni kiongozi kwa mabeki kumshinda MANULA, huyu atatusaidia Sana akiendelea kuaminiwa mwisho wa siku mashibiki mdomo kimyaaaaa!!!...Kama ilivyo kwa kibu tu.

Kama unahisi hajui kadake ww...mtu anacheza goalkeeping kakosea kidogo HAJUI. Yanga wanatuchora tuuu!!!, Sisi tunaendelea kuingiaa Cha kike kila siku kumkataa kipa mzuri.

Manula mda wake unaisha, kuumia sio kwa Bahati mbaya ila ndio ivyo hawezi kurudi kuwa Bora Tena ( hata akirejea atawadakia mpaka lini?? ). Huu ndio ukweli ambao mashabiki wenzangu wa Simba hawataki kuusikia!!

Mpira una mwisho (Ni career fupi) mda ukifika inabidi na wengine wapate nafasi, kwanini hatuigi kwa wenye mpira wao (Europe nk).

Kila siku maswali Ni Yale Yale kwanini CHAMA ajaanza, kwanini phiri achezi, kwanini Manula hakucheza na yupo fiti (alipocheza Vs mtani kwanini amecheza hayupo na hayupo fit...stupid).

Ifike mda tuache Mambo yaendee....tuwaachie wenye profession zao wafanye kazi, sometimes tunajiuliza Nani MCHAWI kumbe mchawi Ni sisi wenyewe mashabiki.

Nawasilisha
Hapo kwenye Phiri hapo ukakasi. Phiri hachezi why?
 
Back
Top Bottom