Awamu ya Tatu:Viongozi wa dini chukueni nafasi zenu

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,291
2,463
Nakumbuka siku ile Rais anatembelea kanisa la maombezi mwa mzee Lusekelo, mchungaji 'alikamua' vibaya mno! Yani alitoa mahubiri yale ambayo ni adimu kwa kuwa mkuu wa nchi alikuweko pale. Alitoa mahubiri yake toka kitabu cha Ester. Katika muktadha huo akisema kuwa watu wenye mamlaka inawapasa kuwa wagumu kushaurika. Wakiwa wanashaurika kirahisi ni rahisi pia kukosea na lawama kwenda kwa mshauriwa na si mtoa ushauri. Hivyo basi mwenye mamlaka anapaswa kuwa 'mbishi' katika kupokea ushauri.

Kadhalika mzee wa upako alisema kuwa hakuna atakayemkejeli hadharani na kumwacha hivi hivi tu. Huyo mtu atausikilizia mziki wake (mzee wa upako).

Pia tuchanganye na ziara za mkuu kanda ya great lakes. Hivyo basi kauli na yale yanayoendelea nchini ni jukumu la mkuu mwenyewe. La msingi ni kuona ni kwa namna gani tunawatumia viongozi wa kidini ili kupunguza hii kasi inayoendelea. Kuna nukuu fulani ya Fidel castro aliwahi kusema kuwa katika harakati zao walifanya mengi. Muda ulilopita walipotazama nyuma miaka kadhaa waligundua kuwa kuna mambo wakifanya kwa maamuzi ya kitoto na mihemko sana. Hata Mw. Nyerere aliwahi kukiri kuwa yapo mambo ya kipuuzi yalifanyika katika utawala wake. Hayo yalikuja kurudiwa na mzee Mkapa aloposema kuwa anajutia sera ya uwekezaji kwani hawakujipanga.

Haya yote hayawezi kuwa somo? Au ndio na wao wanasubiri hadi yatokee ndipo nao wajute? Pengine hawataishia kujuta tu. Ni kweli nchi hii ilihitaji 'dikteta' yaani mtu mwenye uchungu na madhila ambayo nchi nchi hii imepitia. Lakini kwa staili hii ya kunyamazishana ni wazi haikuwa ni matarajio ya wengi.

Itafika wakati mkuu wa nchi atakuwa akiishia kupambana na wapinzani na kusahau malengo yake. Yaelekea pia ndio nia ya upinzani na wanafurahi mkuu wa nchi kucheza mziki wao, na ikifika 2020 watapata la kusema kuwa rais aliishia kuvishighulikia vyama vya upinzani na kusahau wajibu wake kama mkuu wa nchi.

Pengine nami niendelee kushauri kwani ndani ya ccm inaonekana wote wanacbeza midundo ya manju wao. Mkuu ajaribu sana kuziba masikio dhidi ya wapinzani na awaache wafanye wanalotaka huku yeye akiendelea kutekeleza kauli mbiu yake ya hapa kazi tu. Yani namuambia mkuu wa nchi kuwa amewapa rasmi upinzani kazi ya kufanya kwa miaka hii minne hadi 2020.

Kwa nini huwa hawamwelewi baba wa taifa hayati Nyerere alipowashauri ccm waachane na Mrema? Tunaomba kwa nafasi ya kipekee viongozi wa kidini watume timu ya ujumbe kwa rais kuongea nae juu ya uongozi wake na hatma ya Tanzania
 
Kwa kuongezea ni kwamba, mkuu ana maono tatizo ni jinsi ya kuchomoka toka kwenye hicho kiwingu
 
Back
Top Bottom