Awamu ya nne inadekeza udini

dala dala

Senior Member
Nov 16, 2011
106
105
U-dini, U-kabila, U-kanda (Geographical areas) ni baadhi ya mambo ambayo yamesababisha umwagikaji wa damu katika mataifa mengi. Natambua kuna sababu nyinginezo ambazo sijazitaja hapa wasomaji wa makala hii wanaweza kuongeza. Kwa nchini nyingi, hususani Afrika Mashariki ukabila umekuwa chanzo cha misuguano ya kijamii mfano Kenya, Rwanda na Burundi. Hapa kwetu tishio la ukabila, Ukanda si kubwa kulinganisha na U-dini. Nathubutu kusema kuwa, kama kuna bomu linalosubiri kulipuka na kuleta madhara makubwa kwa Watanganyika na Wazanzibar (collectively WATANZANIA) ni machafuko ya kidini hususani baina ya Wakristo na Waisilamu. Sina maana kuwa naombea hili litokee bali kuna dalili kuwa jambo hili lisipokemewa kwa nguvu ya kutosha tutaingia mtegoni. Najua wengi mtapenda kupewa uthibitisho wa maneno yangu, tafadhali pitia mistari hii hapa chini unaweza ukakubaliana nami au vinginevyo;

1. Siku hizi ukitaka kudadisi uwezo wa utendaji wa kiongozi fulani kama wewe ni mkristo na bahati mbaya huyo kiongozi ni muislamu utaambiwa unachuki naye kwa kuwa hampo dini moja.
2. Siasa imengizwa hadi kwenye dini (Igunga Chama tawala kilionyesha wazi wazi kuwatumia waumini wa dini fulani kuharalisha kukubalika kwao
3. Maandamano (mipango ya maandamano) ya dini fulani kushinikiza kupewa upendeleo kwa madai ya kukandamizwa ya dini nyingine.
4. Uteuzi wa viongozi unapofanyika watu wanahoji katokea dini gani (yetu au yao)???

Kimsingi vitu hivi havitoi taswira njema kwa nchi yetu. Mimi wazazi wangu yaani Baba na Mama, mmoja ni Mkristo na Mwingine na muislamu na tunaishi kwa amani na ndugu wa pande zote. Hivyo kimsingi sina sababu ya kuelemea upande wowote ule. Ombi langu kwa Mkuu wa nchi asimamie kidete suala la kupinga roho ya Udini kwani ni hatari sana kwa ustawi wa taifa letu. Mwl. Nyerere na kwa sehemu Alhaji Mzee Mwinyi pamoja na mbabe Mkapa walifanikiwa kuzima moto wa udini. Tatizo kwa huyu mkuu wa sasa anachezea moto kwenye pipa la petroli. Chonde chonde UDINI hautatufikisha popote. NI balaa na janga. Kila mtu aamini anavyoona vema asishughulike na IMANI ya mtu mwingine. Unaweza kuwa na mtazamo tofauti lakini kwa fikra zangu hali si shwari.
 
You have very legitemate concerns about our country's future. All sane people will support your keen observations!
 
Back
Top Bottom