Awali alionekana ni tapeli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Awali alionekana ni tapeli!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  AWALI ALIONEKANA NI TAPELI!

  photos [​IMG] [​IMG]Mtoto Ramadhani Mussa (12) ambaye jana alikamatwa na kichwa cha mtoto mwenzie na kuanza kukinyoya damu hadharani pale kwenye lango la Hosptali ya Taifa Muhimbili, alishawahi kukutwa kwenye makanisa kadhaa ya jijini Dar es salaam akidai kudondoka na ungo na kisha kuombewa na wachungaji wa makanisa hayo, lakini mara ya mwisho alionekana ni kijana tapeli tu au wachungaji waliokuwa wakimuombea walikuwa wanafanya usanii kuvutia 'wauimini'!

  Awali mtoto huyu inadaiwa alikutwa usiku wa manane kwenye Kanisa la Kilutheran pale Manzese na kuombewa na Mchungaji Jonathan wa Kanisa hilo baada ya kudai kuwa amedondoshwa na wachawi wakiwa kwenye ungo, ingawa waumini wengine walimuona kijana huyo kama mchawi na kutaka kumpiga.Baadae inadaiwa alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambako nako alitoweka kimiujiza, kabla ya kukutwa kwenye kanisa lingine Tabata na hatimaye Mikocheni kwa Mchungaji Rwakatare ambako ndiko alipoombewa akiwa na mwenzake kwa muda kabla ya kuambiwa kuwa ni 'matapeli' kwani hizo ndizo zao kujifanya wamedondoka kwenye ungo na kuibukia Makanisani ili kujipatia pesa!

  Akiongea na kituo cha ITV jana, Mchungaji Rwakatare, ambaye pia ni Mbunge wa CCM wa kuteuliwa, alisema "Mungu amejitetea mwenyewe" kwa kuonesha kuwa walichokuwa wanakisema kuwa watoto hao walikuwa na mapepo hawakuwa wanaongopa. Laiti kama wangewaachia wawaombee, yule mtoto asingekufa wala yasingetokea yaliyotokea, lakini kwa sababu kuna watu wanajaribu kuwa kama Mungu, ndiyo maana haya yote yanatokea!

  "Wamuache Mungu awe Mungu", alisema Mchungaji Rwakatare na katika hili amejipatia 'tano' zingine!

  NI STORI YA MWAKA, FUATILIA UNDANI WAKE KWENYE GAZETI LA UWAZI NA MTANDAONI JUMANNE HII!  Dear Guest you have enter our site without being Registered. We recommend to register to view more...
  "Mgeni wetu unatakiwa Kuregista kupata Udaku Wote..."

  http://www.globalpublisherstz.com/2008/04/27/hujifanya_mpoole.html
   
 2. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Huyu mama Rwakatare mwenyewe ndio alikula dili nao ili kulifanya kanisa lake lijulikane kwa kumtumia huyu kijana na kumlipa pesa, kilikua kama kimradi na ili kuonmgeza waumini ambao at the end of the day sadaka pia itaongezeka. hawa wote ni wasanii tu
   
 3. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Mbona hii ni habari ya siku nyingi sana? Kuna jipya hapa kweli?
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  upuuzi mtupu....mods ondoa hii kitu ni ya zamani sana
   
Loading...