Aveva na kundi lako siku zenu simba zinahesabika

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,658
239,132
Simba kukosa tena ubingwa mwaka huu ni jambo ambalo sisi wanasimba hatutakubali , Hii nakujulisha mapema usije kusema tumekuvizia .

Tutakutimua bila huruma , viongozi gani mnaokosa mbinu kiasi hicho ? Hakuna ligi katika miaka mitano iliyopita iliyokuwa rahisi kwetu kama hii , sasa inashangaza sana tunafungwa na timu iliyojaa migogoro na isiyo na kocha wa uhakika kama Azam.

Ni vigumu sana kuwakamata Yanga ( wazee wa fitna ) wakishakaa kileleni , na hili wewe unalijua vizuri sana .

Safari hii tusipobeba ndoo hakutakuwa na Mswalie Mtume , ni heri muondoke wenyewe kwa hiyari yenu .

Simba haiwezi kuwa kichwa cha mwendawazimu.
 
Mbinu atoe Aveva kwani yeye kocha..

Yeye kaajiri makocha kwa kazi hiyo


Mpaka muwaombe radhi familia ya Mafisango ,walifukuzwa kama mbwa chang'ombe

Kaombeni msamaha na mpeleke rambirambi mliyokula

Mpaka mseme pesa ya rambirambi mlipeleka wapi
 
Kama team inapewa kila kitu na wanarukaruka tu unataka viongoz wafanye nini?mchawi wa Simba ni kuamini wanaonewa na kuna team zinabebwa nimeona hata leo na Azam maamuzi sahihi makocha washabik na viongoz wanataka kuingia uwanjani!kuna maamuzi yalikua dhidi ya Azam unaona kabisa wachezaji wa Azam walivyoandaliwa kisaikolojia pale refa anapotoa maamuzi wasiokubaliana nayo
 
Mbinu atoe Aveva kwani yeye kocha..

Yeye kaajiri makocha kwa kazi hiyo


Mpaka muwaombe radhi familia ya Mafisango ,walifukuzwa kama mbwa chang'ombe

Kaombeni msamaha na mpeleke rambirambi mliyokula

Mpaka mseme pesa ya rambirambi mlipeleka wapi
Hii tuhuma aelekezewe Aden Rage , kwanini unatutupia watu wote ?
 
Kwani Simba ni timu ya ukoo ? Achana nayo , kashangilie timu unayoona ni bora,vidonda by tumbo na BP vya nini?
 
Nyie piganeni. Ilikuwa ni wishful thinking kwamba mtachukua ubingwa
Kwa timu ipi hasa?

Kila timu inajua mbinu za Kichuya na hamna plan B. Nani atoke na nani aingie kubadili matokeo? Hakuna?

Endeleeni kujenga timu lakini kiwe Kikosi kipana zaidi. Hilo Kombe la FA mpo kwa hisani ya TFF wanaojali mapato kuliko kanuni!
 
Back
Top Bottom