Auza Ng'ombe kupata fedha za matibabu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
Ngwila_ugonjwa.jpg
Ngwila Daudi
KWA UFUPI
“Kabla sijapata ugonjwa huu nilikuwa nikifanya shughuli mbalimbali na kujipatia kipato change. Niliweza kuitunza familia yangu na kuwasaidia ndugu zangu ambao leo wamenikimbia” anasema Ngwila.

NGWILA Daud (62) ni mkazi wa Kijiji cha Uhambule, Kata ya Igulusi wilayani Mbarali mkoa wa Mbeya ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu alioupata miaka 15 iliyopita na kusababisha uso wake kuvimba.

Ugonjwa huo uliomuanza mwaka 1997, umefanya watu wake wa karibu wakiwamo ndugu na jamaa kumkimbia kutokana na muonekano wake.

“Kabla sijapata ugonjwa huu nilikuwa nikifanya shughuli mbalimbali na kujipatia kipato change. Niliweza kuitunza familia yangu na kuwasaidia ndugu zangu ambao leo wamenikimbia” anasema Ngwila.

Anasema ugonjwa huo ambao uliumiza vichwa vya madaktari katika Hospitali tatu; Hospitali ya Rufaa Mbeya, Ilembula wilayani Njombe na Hospitali ya Igogwe wilayani Rungwe kuutibu, bado haujapata tiba yake hivyo kumfanya aonekana wa ajabu mbele ya watu wengine.

“Ulianza kama upele chini ya mdomo,” anaeleza mwanaye Ayoub Mwalugaje kutokana na yeye mwenyewe kushindwa kuzungumza vizuri.”

Kutokana na kushindwa kuzungumza kwa ufasaha, mwanae Ayoub Mwalugaje ambaye ni mtoto wake pekee alitoa maelezo ya tangu kuanza kuugua kwa mama yake.

Anasema baada ya mama yake kuanza kuugua, ndugu zake walimtenga. “Kilichotusadia kuweza kuendesha maisha ni mali na mifugo iliyoachwa na marehemu baba,” alisema.

Aliendelea “Wajomba zangu wamenitenga mimi na mama. Inaniuma sana kwa kuwa nyakati za usiku mama yangu huwa na maumivu makali, anapumua kwa shida, anatokwa damu puani na mate kwa muda mrefu” anasema Ayoub.

Akisimulia namna anavyohangaika na matibabu ya mama yake, Ayoub anasema mwaka 2002 alimpeleka katika Hospitali ya Ilembula, ambako madaktari walidai kuwa wasingeweza kufanya upasuaji kutokana uvimbe huo kushikana na mishipa.

Anasema baada ya kupata maelezo hayo , alikata tamaa na kuamua kurudi kijijini. Lakini, mwaka 2005 kuna baadhi ya marafiki wa marehemu baba yake walimshauri ampeleke katika tiba za jadi.

Anasema alikwenda katika mji wa Mbalizi ambako alionana na mganga huyo wa tiba za asili (Jina tunalihifadhi). Alimnywesha dawa mama yake na baada ya wiki moja, uvumbe ulipasuka.

“Baada ya uvimbe kupasuka ilitoka damu nyeusi zaidi ya lita mbili, aliendelea kuuguza jeraha na baada ya wiki mbili alipona na kurudi nyumbani huku akiendelea kunywa dawa hizo za kienyeji”.
Anasema uvimbe huo ulipotea kabisa kwa zaidi ya miaka mitatu, lakini cha kushangaza mwaka 2008 dalili za kuanza upya zilianza kujionyesha na baadaye ulianza kuvimba upya.

“Kwa kweli hali ile ilitushtua sana, mara moja tulienda Mbalizi, lakini tulipofika hatukumkuta yule mganga wa kienyeji na tulipojaribu kuuliza watu wake wa karibu hawakuwa na taarifa sahihi alipokuwa amekwenda,” anasema Ayoub.

Anasema wakati akiwa katika harakati za kuokoa maisha ya mama yake, baba yake alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Anasema baada ya kumaliza msiba wa baba yake waliendelea na harakati za kunusuru maisha ya mama yake na safari hii walimpeleka katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Anasema baada ya uchunguzi wa kina, madaktari walidai kuwa uvimbe ule umesababisha saratani. Lakini hawakuwa na uwezo wa kutibu na kumshauri atafute hospitali zenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Auza Ng’ombe kupata fedha za matibabu

Anasema baada ya kuuza zaidi ya ng’ombe 10, alimpeleka mama yake katika Hospitali ya Igogwe wilayani Rungwe na walipomfanyia uchunguzi walidai uvimbe huo ni tezi na si saratani hivyo matibabu yake yanahitaji umakini mkubwa.

Anasema maelezo hayo ya wataalamu katika hospitali hizo, yamefanya kubaki njia panda, kwa kuwa licha ya kuona uvimbe huo ukimtesa mama yake, ni ugonjwa gani na matibabu yake ni yapi.

“Tumehangaika sana sehemu mbalimbali lakini hatujapata suluhu, na kwa kuwa tumekuwa tukisikia kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuna watu wanaweza kuifanya uchunguzi wa kina tumeona tuombe msaada kwa jamii,” anasema Ayoub na anaongeza;

“Naomba Watanzania wenzangu wanisaidie kunichangia chochote naamini kwa msaada wao nitaweza kujua mama yangu anaumwa nini, ili aweze kupatiwa matibabu na kupona kabisa.”

Mtu yeyote aliyeguswa na mada hii na anahitaji kumsaidia, anaweza kuwasiliana kwa simu yake namba 0768 75 37 24 au kutuma mchango wake wowote. Auza Ng'ombe kupata fedha za matibabu - Kitaifa - mwananchi.co.tz







 
Kabla hujafa hujaumbika,inasikitisha sana,kwa kua kuna namba za mawasiliano kila mmoja wetu kwa nafasi yake naamini ataguswa na kuangalia ni kwa namna gani tutamsaidia.
 
Back
Top Bottom