Ndugu yangu huyu jamaa yuko kazini kwa hiyo inambidi awahi kurusha propaganda za Kigali katika masuala yote ambayo kigali imecheza faulo ili propaganda hizo zifunike ukweli. Maswali ya kujiuliza ni:
1. Alipochinjwa mpinzani Andre kagwa rwisereka, serikali ya Rwanda ilikataa kuruhusu ndugu zake wasafirishe mwili nje kwa ajili ya independent autopsy, wakidai eti itaingilia usalama wa taifa la rwanda!!! Hivi inaingia akilini kweli? Kwani ndugu ni wa serikali? Serikali ililazimisha azikwe hivyo hivyo kwa autopsy ambayo ndugu zake hawakubaliani nayo chini ya mtutu!
2. Alipouawa Seth sendashonga nchini Kenya mbona hawakutaka mwili urudishwe Rwanda wafanye autopsy?
3. Alipouawa Theogene turatsinze nchini mozambique mbona hawakutaka mwili urudishwe Rwanda wafanye autopsy?
4. Alipouawa Charles Ingabire nchini Uganda mbona hawakutaka mwili urudishwe Rwanda wafanye autopsy?
5. Alipouawa Patrick Karegeya nchini South Africa mbona hawakutaka mwili urudishwe Rwanda ili wafanye autopsy?
6. Alipouawa Theoneste Lizinde nchini Kenya mbona hawakutaka mwili urudishwe Rwanda ili wafanye autopsy?
7. Alipouawa Augustin Bugirimfura nchini Kenya mbona hawakutaka mwili urudishwe Rwanda ili wafanye autopsy?
Je hawa wote hawakuwa wanyarwanda kama alivyo balozi Bihozagara? Ukweli ni kuwa Rwanda inajua exactly nini kimemuua balozi haya ni maigizo tu. Haiwezekani serikali iliyokataa kumpa passport BALOZI wake mwenyewe KWA MIAKA SITA, ndio leo iwe ina uchungu sana naye kiasi cha kurudisha mwili nyumbani na kufanya autopsy ya serikali kana kwamba alikuwa Burundi kikazi! Serikali ya kawaida inayojiheshimu ingesusa kwa sababu mhusika kwa miaka sita alikuwa anakaa nchi ya watu kama mkimbizi haramu akiitia aibu Rwanda kuwa hakukaliki! Wanajifanya kufanya autopsy wakati Burundi imeshasema kilichomuua ni kitu gani.
swali kwa
mchambawima1: unakumbuka kuwa aliyekuwa balozi wenu nchini Netherlands ndugu Jean pierre bizimana alikimbia kazi yake na kuomba ukimbizi wa kisiasa nchini Ireland? Na sababu aliyotoa ni kuhofia kuuawa baada ya kukataa amri kutoka Kigali ya kutumia hadhi yake ya kibalozi kufanikisha mauaji ya Victoire Ingabire wakati Ingabire alipotangaza kutaka kurudi Rwanda kuwania urais?
Je unakumbuka kuwa ALIPEWA! Je kwa nini Rwanda hailalamiki kuwa kitendo cha Ireland kutoa hadhi hiyo ya ukimbizi wa kisiasa inayotambulika na UN kwa sababu kama hiyo ya kutaka kumuua Ingabire akiwa Netherlands ni uchochezi?
cc:
Sethshalom