Australia yatoa Tsh. bilioni 60 kuisadia Tanzania kwenye miradi ya umeme jua

Australia yatoa Tsh. bilioni 60 kuisadia Tanzania kwenye miradi ya umeme jua

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Serikali ya Austria kupitia Benki ya UniCredit imeahidi kuipatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha Euro milioni 20 (sawa na takribani Shilingi bilioni 60) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mipya ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua na taka.

Soma pia: Ajira 31,148 zimezalishwa kwenye miradi ya umeme

Screenshot 2025-09-18 055734.png

Ahadi hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Merl Solar Technologies GmbH, Mhandisi Hannnes Merl, alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Septemba 17, 2025, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 69 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic (IAEA) unaoendelea jijini Vienna, Austria.

Mhandisi Mramba ameikaribisha kampuni hiyo nchini Tanzania kwa ajili ya kukutana na wataalamu na kuanza maandalizi ya utekelezaji wa miradi hiyo mipya, huku akiahidi ushirikiano wa karibu katika kufanikisha hatua zote muhimu.

Amebainisha kuwa kampuni ya Merl tayari imetekeleza miradi kadhaa ya umeme wa jua nchini, ikiwemo miradi iliyotekelezwa kati ya mwaka 2015 hadi 2017 katika vijiji 10.

“Mradi huo ulihusisha makontena 14 ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika Wilaya za Kongwa (Dodoma), Mlele (Katavi) na Uyui (Tabora) kwa gharama ya Shilingi bilioni 16.2,” amesema Mhandisi Mramba.

Manufaa yaliyopatikana
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, miradi hiyo imewezesha:

Nyumba na makazi 812 kuunganishiwa umeme,
Nyumba za ibada 27 kupata huduma ya umeme,
Shule 6 kuunganishwa, na
Vituo vya afya 8 kupata nishati ya uhakika.
 
Back
Top Bottom