Atychiphobia

dume30

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
567
Reaction score
577
Umewahi kusikia hilo neno "Atychiphobia"? Atychiphobia ni tatizo la kisaikolojia linalotokana na hofu ya kupitiliza ya kufeli jambo lililo mbele yako ,Yaweza kua mtihani au Usahili wa kazi.

Watu wengi upatwa na tatizo hili hususani wanafunzi.
Kwa muktadha wa leo sitajikita kwenye hofu ya kukosa usahili wa kazi bali ntajikita kwenye Hofu ya kufeli mtihani ambayo uwakuta wanafunzi wengi.

Andiko hili ni mahsusi kwa wazazi wenye watoto wanaolekea kwenye mitihani ya kidato cha nne,,Waweze kulielewa tatizo na kujua namna ya kuweza kusaidia vijana wao kama si kuiondoa hofu hiyo basi walau kuipunguza.

Nini hasa kinaweza kuleta/kusababisha hofu hii?

1. Historia ya familia,Hapa nitaeleza mazingira mawili tofauti kuhusu familia,la kwanza kama kwenye familia kuna historia ya watu kua waoga wa mtihani/kukimbia mitihani,historia ya tatizo la afya ya akili na msongo wa mawazo kijana wako yupo hatarini kukutwa na hofu hii hivyo unahitaji kumuandaa mapema kisaikolojia na kihisia.
Upande wa pili kuhusu historia ya familia mara nyingi watoto ambao ndugu waliowatangulia kwenye familia wamekua wakifeli mitihani hususani ya Taifa,Na kijana wako ndo anafata kwenye huo mstari ni rahisi kupata hofu hii kuliko yule ambaye watangulizi wake(dada zake na kaka zake) wote wamekua wakifaulu,kufaulu kwao kutamsaidia kumtolea au kumpunguzia hofu ya kufeli badala yake itamjengea confidence japo kua hii pia sio karata itakayomfanya nae afaulu kwakua tu kaka na dada walifaulu bali hawezi kua na hofu ya mtihani ukilinganisha na wa kwanza.

2.Tabia za kujifunza/mazingira, Mwanafunzi aliyekulia katika mazingira ambayo watu wanafundisha au wanaamini kufeli ni jambo lisilokubalika katika jamii na hakuna linalowezekana baada ya kufeli mtihani atakua na tatizo hili la kuogopa mitihani kupitiliza, hili pia linaweza sababisha tatizo hili la hofu ya kufeli.

3.Uwepo wa Hofu nyengine, Wakati mwengine kama si mara zote hofu zinaweza kutokea pamoja, au hofu fulani inaweza kusababisha hofu nyengine itokee, Mfano mwanafunzi muoga wa shule(mwenye hofu ya shule) kitaalam scolionophobia anaweza pia kua na tatizo hili letu Atychiphobia la kuogopa kufeli mtihani, ni wazi aliyekua anaogopa shule maana yake mara nyingi alikua haendi shule au anatega ,Mitihani ikifika haswa hii mikubwa ya kitaifa lazima awe na hofu ya kufeli,Hofu ya kwanza imepelekea hofu ya pili kutokea.

4.Uzoefu wa kiwewe(Traumatic experience),
Kama mtoto ana kumbukumbu ya kipigo,kuumizwa ,kuteswa,kulazwa njaa ama kunyimwa mahitaji yake ya msingi kisa tu alifeli mtihani fulani,Hili pia linaweza kuleta hofu hii ya kufeli mtihani au kuukimbia kabisa mtihani wenyewe.Hii inamaana gani kwa wazazi? Adhabu kali kwa mtoto mara baada ya kufeli mtihani fulani haitamjenga zaidi mtoto kwa mtihani ujao bali adhabu hizo zitamharibu.

Naishia hapa kwasasa,Kesho ntaweka bandiko la namna ya kumsaidia mtoto mwenye tatizo hilo.
Nakaribisha maswali pia.
 
Ahsante nasikita umepata comment moja tu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Nashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…