Attack za CCM Mtandao vs. CHADEMA Mtandao

ushauri mzuri sana Junior Zito..Nasikia kaka yupo nje ya nchi kweli haya..joking?
Haaahaaaa mkuu unanikumbusha kisa cha zitto kule sumbawanga.....asee huyo jamaa hta kma mie polisi siendi kumkamata 😀😀😀😀
 
Hili Jukwaa limeharibika baada ya Uvccm walipojua ukiwatukana viongozi wa Upinzana wanaku Makonda.yani unateuliwa ndio maana umeona ukiongea baya kuhusu Serikali hawa Uvccm wanakujibu km wao ndio wasemaji.
 
Tatizo ni kwamba wengi wanaounga mkono ccm hapa jf ama watoto wa viongozi au wake zao , ama ni viongozi wenyewe , kwahiyo wako tayari kufa kwa ajili ya maisha yao yanayotegemea kudra za ccm .
 
Sure
 
Naunga hoja mkono.ingawaje hili ni jukwaa la siasa leo hii limebadilika na kuwa la vyama viwili. Ccm na chadema. Hii inaleta mkanganyo sana kwani kwa asiye na chama matusi ,kejeli vitakuishia. Kuna baadhi ya majukwaa wako smart sana,wanabishana kwa hoja bila kejeli wala matusi,ni bora sasa wanaojiita timu lumumba au timu ukawa kubadilika ili hata kwa ambao siyo wanasiasa kuweza kujiunga na chama fulani kupitia hoja zinazitolewa hapa
 
Huu Uzi c wa kichama lakn kunabaadhi ya comment zimeingia uchama zaidi ila Luna baadhi ya watu kutukana ni moja ya maisha yao katk jamii.

Kiukwel nimekuwa nikisoma threads mbali mbali cjawahi kuona Uzi wowote ule unaoelezea maendeleo na jinsi ya kujifunza maendeleo na jinsi gan maendeleo yanapatikana watu wamekuwa uccm uchadema mpaka kelo wengne hatu vyama kabisa na c washaabiki wa vyama. Mm ningeomba kila mtu Ajitambue kiukwel kikwel maswala ya siasa yametuchosha wengne na hili swala vijana wasio kuwa na maada za mcng wakae pembeni kiikwel
Na kunakitu k1 nimekigundua humo JF mtu akianzisha thread ya kizungu wachangiaji ni wachache cn weng wao watabakia kupita tu au kuandika tuneno 2 tu kwa muda mwingne tubadili hata lugha tuone matuc yatakuwepo
 
Vijana wa kizazi hiki wengi wamewakabidhi wanasiasa zao
 
Hill jukwaa limevamiwa na watu ambao think capacity haifikilii kingne nahc weng wao ni wanaoshinda kwenye vibanda vya magazeti kusoma vichwa vya habar vya magazeti
 
Vijana wa CCM na CHADEMA kwakweli wanaharibu maana halisi ya "Home of Great Thinkers"
Asilimia kubwa sana hatutumii akili zetu vizuri.
Utashangaa mtu akileta mada ambayo haihusiani na siasa wachangiaji watakuwa wachache sana.
Let's use our heads guys....
 
Kuna wanasiasa tuliwaambia kipindi kile kuwa walimu wamegoma mgomo mrefu, wanasiasa wakapinga wakiwapa vitisho kisha kuwalaghai.
Wakawalazimisha watoto wafaulu, walimu wakatii kisha wakaanza kutemgeneza kizazi cha watoto wawezao kufaulu mitihani ya taifa huku wakikosa stadi nyingi.

Kizazi hicho kimeendelea hivyo hivyo na kilivyokutana na upepo wa siasa vikakumbwa nao na ndicho kinachosumbua sahizi.
Hicho hakipingi kwa hoja , bali hupinga hoja kwa kuwatusi watoa hoja, kuwakashfu hata kudharau, kimetiwa upofu wa vyama vya siasa wanavyoviamini huku wakiona kuamini tofauti na wanavyoamini ni Upumbavu ama dhambi kubwa wakati mwingine wakitamani wabaki wao pekee(yaani chama wanachokiamini)

Hao ndio wanaofurahia vifo vya watu wanaoamini vyama tofauti na wanavyovifuata, wapo tayari kuwatusi wazazi wao ama jamaa zao kisa wanaamini tofauti na wanavyoamini hawana nafasi ya kuelimisha na kushawishi maana hawajawahi kuelimishwa ama kuelimika, wamefanya vyama ni dini ama imani.

Na bahati mbaya kizazi hicho kinaendelea kuendelezwa kwani hao wanaenda kuwa walimu , walezi , wazazi na viongozi. Hakitakoma kwani ni kama ugonjwa wa urithi uendao vizazi na vizazi.


Demokrasia ni kama wimbo wa msibani, haufurahishi na wala haupendwi ila ipo siku kama hutouimba, utausikia na usipousikia utaimbiwa
 
Kiapo cha nitasema ukweli daima ni kiapo cha TANU,CCM kwao zidumu fikra za mwenyekiti hivyo hata kama utakuwa msomi fikra zako na mawazo huru unafukia ardhini.


Wew jamaa yani tayari ushaanza siasa tena! Kweli jf ya sasa si kama ile ya zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…