My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,293
Wakuu salamu.
Kwanza natanguliza Samahani Kwa mtu yeyote au watu watakaokereka na hili post yangu, lengo ni kuelimishana, Kama ilivyo kawaida ya JF tunapeana maarifa mbalimbali.
Majina huwa ni roho kamili usiyoweza kuiona Kwa mwili wa damu na nyama, lakini yanaishi ktk ulimwengu halisi tulionao Kwa matendo kabisa.
Ukimwita mtoto jina la kurithi la babu yake ambaye pengine alikuwa mchawi, ni lazima huyo mtoto atafuata tabia za babu yake kwa maana ya roho kufuatilia jina lake.
Kwa mfano mtoto akiwa Masumbuko, basi tabia zake zitakuwa za kimasumbuko tu, mnamkumbuka mwanasiasa machachari Sana miaka ya 1990 aliyekuwa akitetemesha bunge na serikali, lakini kutokana na jina lake akawa amepotea tu na sijui yuko wapi Siku hizi.
Ukimwita mtoto Burundi, atakuwa Kama taifa la Burundi lilivyo.
Ukimwita mtoto Tanzania, pia atakuwa na tabia na hulka zote za Tanzania maana roho inatafuta kutimiza mambo yake.
Ukimwita mtoto Canada, naye atakuwa Kama Canada.
Ukimwita mtoto Rwanda, hakika atakuwa Kama Rwanda ilivyo.
Ukimwita mtoto Makonda, naye atakuwa Kama mh Makonda alivyo au atafuata tabia za kina Makonda kulingana na ukoo wao.
Ukimwita mtoto Jakaya, naye atakuwa Kama Jakaya au kulingana na ukoo wao wa jina ulivyo.
Ukimwita mtoto Trump, naye atakuwa Kama Trump au kulingana na ukoo wao ulivyo.
Ukimwita mtoto Kenya, naye atakuwa Kama taifa hilo lilivyo.
Kuna mtoto mmoja hapa mtaani ninapoishi anaitwa Marekani, huyu mtoto ni mgomvi sijawahi kuona, ana umri wa miaka 4 tu lakini anapigana hadi na watoto wa miaka 10,na tena huwafuata makwao akiwa kabeba mawe.
Kuna jamaa mmoja alifuga mbwa akampa jina la Gaddafi, huwezi kuamini huyo mbwa ni mbabe Sana Kwa mbwa wenzake na ajabu akiwa anakula si mchoyo Kwa wenzake.
Ukimwita mtoto Shida hakika ataishi maisha ya shida tu, ktk ulimwengu wa roho, ni lazima kwanza uvunje madhabahu za kichawi, kiganga, kimizimu, kiukoo ambazo zilinenewa kuhusu hilo Jina, na njia nzuri ya kuvunja ni kupitia maombi tu na wala siyo uchawi,hapo ndo unaweza kumiliki jina ulilopewa pasipo kukuletea matatizo.
Lakini inatakiwa yawe ni maombi ya nguvu hasa, ila si rahisi sana kuvunja madhabahu yenye majina ya nchi japokuwa inawezekana.
Maana kila taifa lina maunganiko yake, kuna mataifa yameunganishwa kuzimu na ndo maana hayana amani kila leo na au yamejaaa dhiki tupu Kwa raia wake hata Kama yana raslimali kiasi gani.
Na kuna mataifa yameunganishwa na Mungu moja Kwa moja hayana raslimali lakini raia wake hata wasio na ajira wanapewa posho Kwa mwezi ya kujikimu na ugumu wa maisha.
Kwa hiyo ukimwita mtoto Finland, au Norway au Sweden hakika atafanana tabia Kama hayo mataifa na siha yake ya kimaisha itafanana na taifa husika.
Tofauti na ukimwita Burundi au Angola, Kama huamini jaribu uone.