Athari za kula chakula huku ukishushia maji hapo hapo(Kwa wanaume)

Squidward

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
7,692
9,322
hodi madokta sorry kuna ndugu yangu hapa mwanaume anapenda kula na kunywa maji hapo hapo je kuna tatizo lolote litalomtokea?

asante
 
Yah uko sahihi mkuu....naweza sema madhara yake sio makubwa...lakini ni muhimu to take time before or after meal atleast half an hour au zaidi kwasababu maji hasa yakiwa mengi yata slowdown digestion process(umengenyaji wa chakula) kwa kudilute enzymes(vimengenya) kuanzia kwenye tumbo ambapo proteins huanzwa mengenywa na huwa inaitaji sana hali ambayo ni asidi(acidic medium around 3-2 ph) hivyo apo italeta shida kidogo.

Vile vile yanaspeedup the movement food materials katika gastrointestinal tract(njia ya chakula) hasa from stomach na kwenye utumbo mdogo(including duodenum ,jejunum na ilium) ambako kwa asilimia zaidi ya 95 ndo umeng'enyaji (digestion) hufanyika hivyo mwili hushindwa kunyonya virutubisho(food substrates) toka kwenye chakula icho ilichokula.

Na mara nyingi unakuta muda si mrefu unaanza kujisikia njaa tena.

Vilivile hata tunapokula matunda tusile mda mfupi baada ya chakula au kwa pamoja haitakiwi.....ni bora kula mda kabla ya meal au mda baada ya meal.
 
hodi madokta sorry kuna ndugu yangu hapa mwanaume anapenda kula na kunywa maji hapo hapo je kuna tatizo lolote litalomtokea?

asante
Wee unaitwa nani? Inawezekana mi ndo huyo ndugu yako, mimi nikila, kila baada ya vijiko kadhaa lazima ninywe maji. Mpaka namaliza kula naweza nikawa nimekunywa karibu lita moja.
 
yah uko sahihi mkuu....nawesa sema madhara yake sio makubwa...lakini ni muhimu to take time before or after meal atleast half an hour au zaidi kwasababu maji hasa yakiwa mengi yata slowdown digestion process(umengenyaji wa chakula) kwa kudilute enzymes(wimengenya) kuanzia kwenye tumbo ambapo proteins huanzwa mengenywa na hua inaitaji sana hali ambayo ni asidi(acidic medium around 3-2 ph) hivyo apo italeta shida kidogo.....vile vile yanaspeedup the movement food materials katika gastrointestinal tract(njia ya chakula) hasa from stomach na kwenye utumbo mdogo(including duodenum ,jejunum na ilium) amboko kwa asilimia zaidi ya 95 ndo umengenyaji(digestion) hufanyika hivyo mwili hushindwa kunyonya virutubisho(food substrates) toka kwenye chakula icho ilichokula.....na mara nyingi unakuta mda si mrefu unaanza jisikia njaa tena.....
vilivile hata tunapokula matunda tusile mda mfupi baada ya chakula au kwa pamoja haitakiwi.....ni bora kula mda kabla ya meal au mda baada ya meal.....
Hapa kuna point, asante! Mimi hunywa sana maji wakati nakula kama mleta mada alivyosema, ila masaa machache baada ya kula husikia njaa.
 
Dk.Ndodi alinichambulia hii siku moja.yapo mengi ikiwa pamoja na usingizi mzito baada ya kula
 
Ila mbona tunakunywa chai/liquids na vitafunwa (during breakfast) vikiambatana..!?

*Hizi tafiti za sayansi ni jipu maana kuna mda naonaga ni mtu anaamua tu kueka ideology yake na si kwamba its proven from different spicemens.
 
Unapokunywa maji baridi na huku unakula , una solidify oil into fats ambazo digestion yake ni ngumu
 
hodi madokta sorry kuna ndugu yangu hapa mwanaume anapenda kula na kunywa maji hapo hapo je kuna tatizo lolote litalomtokea?

asante
dah!
sasa anapokula ugali akazimua na maji si ni sawa na kunywa uji!
itakuwa haina madhara labda uniambie uji sumu kwa wanaume.
 
Hapo hapo je inaweza kuwa kunachangia mtu kuwa na kitambi kutokana na kula na kunywa maji baridi kabla ya nusu saa.?

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Wee unaitwa nani? Inawezekana mi ndo huyo ndugu yako, mimi nikila, kila baada ya vijiko kadhaa lazima ninywe maji. Mpaka namaliza kula naweza nikawa nimekunywa karibu lita moja.


Labda tuna undugu ila id zetu ni mafumbo ili tusijuane afu tukanuniana
 
Tatizo la kujamba jamba hovyo bila breki.

Unajaza upepo ndani ya tumbo wakati wa kula na kusababisha chakula kutokusaga vizuri, matokeo yake ni kujamba jamba hovyo hovyo

Ushauri wako mzuri ila unavunja mbavu hahahah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom