Nikiwa kama mwananchi mzalendo, nimetafakari sana athari tutakazozipata kutokana na ahadi zinazotolewa katika majukwaa ya siasa hasa katika kipindi hichi cha kampeni.
Baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiahidi mambo ambayo ukiyaangalia kwa undani hayawezi kutekelezeka hata kidogo.
Tumemsikia Mgombea wa Urais Zanziba kwa tiketi ya ACT Wazalendo Maalim Seif Hamad akitoa ahadi kuwa atapandisha kima cha chini cha mishahara hadi kufikia silingi Laki 5 za kitanzania. Ikumbukwe kwamba kima cha chini cha mishahara kinapandishwa Serikalini kinaenda sambamba na kile katika sekta binafsi.
Je, Ni sekta binafsi ngapi zina uwezo wa kupandisha kwa kiasi hicho? Je, Bajeti ya serikali ya Zanziba inaakisi upandishwaji wa mishahara kwa kiwango hicho? Je, vyanzo gani vya mapato vitatumika kama sio kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Pia, baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia majukwaa kuubeza Muungano wetu wa Tanganyika na Zanziba ambapo wamekuwa wakiuelezea kwa lengo la kupotosha ukweli na uhalisia wake.
Wazanzibar na Watanzania bara kwa ujumla tusiingie katika mtego huo kwani kwa kushirikiana kwetu tumepata Nchi ya neema Tanzania, na chokochoko zote zinazoendelea zina lengo la kuhakikisha wanawaingiza wananchi kwenye machafuko.