Athari Kuu Kiuchumi:Mbinu Za Utumbuaji Majipu-Bandari

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Napongeza kwa dhati na kwa heshima kubwa jitihada zinazofanywa na Serikari ya awamu ya Tano hasa ktk usimamizi wa vyanzo vya mapato ya nchi na misingi ya maadili,uchapa kazi ,kujituma na uzalendo.

Zipo athari kadhaa zinazojitokeza kutokana na namna majipu makubwa kwa madogo yalivyotumbuliwa..hasa ukizingatia macho ya husuda,faraka,fitina na chuki toka kwa baadhi ya majirani na washindani wetu katika fulsa za kimataifa kibiashara kama bandari,barabara na n.k

Mathalani suala la Bandari ambako taarifa za wizi,ubadhirifu,upotevu wa mizigo {wizi wa Makontena} zimetolewa kwa nyakati tofauti na kutangazwa na vyombo vya habari vya ndani ya nchi na nje ya nchi.Kifulsa marafiki na majirani zetu kiuchumi/Kisiasa wametumia mwanya husika kama point of strength kuwashawishi wateja kimataifa kutotumia miundombinu yetu {ports gateways} kuagiza ama kusafirisha nje {imports and exports },Moja ya hoja wanazotumia ni hatari za kiusalama ,uaminifu, {credibility,Intergrity,ethics}.

Tuhuma madhubuti zimegusa maafisa waandamizi katika Mamlaka ya Bandari,Maafisa waandamizi mamlaka ya mapato,Makampuni ya uwakala wa Forodha,Wamiriki wa bandari kavu na N.k......Taarifa zisizo rasmi zinaonyesha tayari kuna upungufu mkubwa wa mizigo inayopita katika bandari {Dar es salaam/Tanga/Kigoma} zetu moja ya sababu ikiwa tuhuma za wizi na Mfumo wa Single Customs Territory.

Mungu mwema awajalie hekima zaidi na busara zaidi washauri wa viongozi wetu ili kila hatua wanazochukua zisiwe na athali kubwa sana kwa nchi leo na kesho
 
Napongeza kwa dhati na kwa heshima kubwa jitihada zinazofanywa na Serikari ya awamu ya Tano hasa ktk usimamizi wa vyanzo vya mapato ya nchi na misingi ya maadili, uchapa kazi , kujituma na uzalendo.

Zipo athari kadhaa zinazojitokeza kutokana na namna majipu makubwa kwa madogo yalivyotumbuliwa..hasa ukizingatia macho ya husuda,faraka,fitina na chuki toka kwa baadhi ya majirani na washindani wetu katika fulsa za kimataifa kibiashara kama bandari,barabara na n.k

Mathalani suala la Bandari ambako taarifa za wizi,ubadhirifu,upotevu wa mizigo {wizi wa Makontena} zimetolewa kwa nyakati tofauti na kutangazwa na vyombo vya habari vya ndani ya nchi na nje ya nchi.Kifulsa marafiki na majirani zetu kiuchumi/Kisiasa wametumia mwanya husika kama point of strength kuwashawishi wateja kimataifa kutotumia miundombinu yetu {ports gateways} kuagiza ama kusafirisha nje {imports and exports },Moja ya hoja wanazotumia ni hatari za kiusalama ,uaminifu, {credibility,Intergrity,ethics}.

Tuhuma madhubuti zimegusa maafisa waandamizi katika Mamlaka ya Bandari,Maafisa waandamizi mamlaka ya mapato,Makampuni ya uwakala wa Forodha,Wamiriki wa bandari kavu na N.k......Taarifa zisizo rasmi zinaonyesha tayari kuna upungufu mkubwa wa mizigo inayopita katika bandari {Dar es salaam/Tanga/Kigoma} zetu moja ya sababu ikiwa tuhuma za wizi na Mfumo wa Single Customs Territory.

Mungu mwema awajalie hekima zaidi na busara zaidi washauri wa viongozi wetu ili kila hatua wanazochukua zisiwe na athali kubwa sana kwa nchi leo na kesho
Fulsa = Fursa.
MKuu ulitaka serikali ichukue hatua kimya kimya??
Hivi unajua hasa namna wizi unavyotokea pale TPA??
Issue sio kwamba wateja hawapati mizigo yao, hiyo ni kesi ingine tofauti kabisa. Pale TPA ni kua wateja wanapata mizigo yao ila Kodi ndio haiingii serikalini.
 
Ningewashauri wangeendesha utumbuaji huo kimya kimya bila makelele....! Wakumbuke Simba mwenda pole ndie mla nyama.....
 
Upungufu wa mizigo umesababishwa na kufungwa mianya ya upigaji mkuu, wale waliokuwa wanafanya biashara kiujanja ujanja ndo wameacha kuagiza mizigo wanasikilizia kwanza
 
Yamkini upo sahihi japo vema tujiongoze vema kufahamu nani hasa wateja wakuu katika utumiaji bandari zetu,je ni Watanzania?Wageni? The truth remain kwamba wageni ndio watumiaji wakubwa wa bandari zetu ..na wao hawawajibiki kulipa kodi kuu zozote zaidi ya tozo ndogo na za kati...Ingawa pia kuna ukweli kwamba waagizaji wengi wa ndani ya nchi wanatuhumiwa kushirikiana na maafisa wa mamlaka ya mapato na mawakala forodha kuagiza mizigo kana kwamba mizigo inakwenda nje ya nchi lakini uishia kuuzwa ktk soko la ndani pasipo kulipiwa kodi stahili.
 
Back
Top Bottom