mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,609
- 10,640
Wadau heshima kwenu
Mtakumbuka kumekuwa na kelele nyingi za kuhoji uhalali wa wabunge wetu kulipwa ile posho yao ya makalio. Wananchi hawataki kusikia posho kama hiyo ikiendelea kulipwa. Sababu ni ya msingi kabisa. Ni posho wasiyo stahili kulipwa kwani tayari wanalipwa per diems. Kwa maneno mengine ni double payment, which is fairly not acceptable. Sababu ya pili ni kwamba ifutwe kwavile posho za vikao za wafanyakazi wengine tayari zimefutwa. So ni double standard kama wabunge wataendelea kulipwa hiyo posho.
Mheshimiwa Zitto Kabwe na Mhe. Elibariki Kingu angalau walijaribu kuonyesha kuwa hii posho si fair kwa wabunge kulipwa. Kuna karoho fulani kauzalendo kanawasuta! Lakini kwa vile malipo yanatolewa basi wao wakaona bora wazielekeze kwenye miradi ya wananchi moja kwa moja. Kwa maana nyingine wanawarudishia wananchi kile kilichoongezeka. Sasa najiuliza ni nani kati ya hawa wabunge ataibeba hoja hii kuipeleka bungeni ili hii 'posho chukizo kwa wananchi' ifutwe moja kwa moja?
Maoni mbalimbali ya wadau humu yamekuwa yakimtaka Mhe. Rais Magufuli aifute hii posho kama alivyofuta zile za makazini na ile ya kamati za bunge. Lakini baadhi ya wadau humu humu wamekuwa na hoja kwamba Mh. Rais hana ubavu wa kuifuta hiyo posho kwa vile iko kwenye kanuni za bunge, so ni hali kanuni husika ibadilishwe. Hapa naombeni kuelemishwa ni kanuni gani hiyo ya bunge inayotaja hii posho? mi nimesoma zile kanuni za kudumu za bunge lakini sijaona kitu hiki, labda kama niliruka kipengele unknowingly. Kwa aliyesoma hiki kifungu atusaidie tafadhali.
Nawasilisha