Assad: Shambulizi la kemikali lilikuwa ni uwongo asilimia 100

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
_95632373_mediaitem95632370.jpg


Rais wa Syria Bashar-al Assad, anasema kuwa ripoti za shambulizi la silaha za kemikali lililofanywa na jeshi lake lilikuwa ni uwongo kwa asilimia mia moja.

Katika mahojiano ya kipekeke na kituo cha Agence France-Presse, Assad alisema kuwa hakukuwa na amri ya kufanywa shambulizi lolote.

Zaidi ya watu 80 waliuawa katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Khan Sheikhoun tarehe 4 mwezi Aprili, na mamia kupata matatizo yaliyosababishwa na kile kinachotajwa kuwa shambulizi la kemikali.

Walioshuhudia walisema kuwa waliona ndege zikishambuaia mji huo lakini Urusi inasema kuwa ghala la silaha la waasi ndilo lilishambuliwa.

Picha za kushagaza zilionyesha waathiriwa wengi wao wakiwa ni watoto wakitokwa na pofu mdomoni.

Walioathirika walipelekwa hospitalini nchini Uturuki inayompinga rais Assad

Tangu wakati huo Uturuki ilisema ina ushahidi kuwa silaha za kemikali zilitumiwa,.

Bwana Assad anasema kuwa nchi za magharibi zilibuni taarifa hiyo kama kizingizio cha kufanya shambulizi la ndege katika kituo cha wanahewa wa Syria, shambulizi hilo lilifanyika siku chache baadaye.

Urusi, mshirika mkubwa wa Syria iliwagadhabisha Marekani, Uingereza na Ufaransa siku ya Jumatano, kwa kupinga msuada ambao ungeruhusu serikali ya Assad kutoa ushirikiano kwa uchunguzi kuhusu kile kilichotokea.

Chanzo: BBC
 
I Chemical ‘attack’ was false flag to justify strike on airbase – President Assad

Published on Apr 21, 2017Syrian President Bashar Assad warned that what he called “false flag” incidents and provocations, similar to the one he said took place in the town of Khan Shaykhun, are likely to occur in future to give the US a pretext for an attack.
the stranger things not even one American Jew controlled TV showed this interview to the American peoples and the rest of the world to see the reality
 
Back
Top Bottom