GE2025 Askofu Msoganzila: Uchaguzi ufanyike kwa haki na amani. Nendeni mkapige kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma mkoani Mara, Michael Msoganzila leo Oktoba 26, 2025 amewaomba waumini wa kanisa hilo kuombea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Jumatano Oktoba 29, 2025 ili uwe wa haki na amani na kuwahimiza kwenda kupiga kura na kuchagua kiongozi wanayeona anafaa kwa maendeleo.

Your browser is not able to display this video.
 
..utafanyika vipi kwa haki ukizingatia dhuluma iliyofanyika mpaka sasa hivi?

..uchaguzi ni mchakato na mauzauza yameanza muda mrefu na yanahitimishwa Oct 29.
 
..utafanyika vipi kwa haki ukizingatia dhuluma iliyofanyika mpaka sasa hivi?

..uchaguzi ni mchakato na mauzauza yameanza muda mrefu na yanahitimishwa Oct 29.
Sisi Jumatano tunaenda kupiga kura wewe baki nyumbani kwako mkuu.
 
Reactions: Tui
Askofu wangu usitake utukanwe
Kupiga kura kuwashindanisha akina nani.
Usitake utukanwe wakati unaheshimika sana.
 
Padiri kapige kura mwenyewe, mie kura yangu sijui kama hata kama ninayo au walishaiiba!
 
Sisi Jumatano tunaenda kupiga kura wewe baki nyumbani kwako mkuu.
Huu uchaguzi watashiriki mashetani na wazao wao.

Wapiga kura wametekwa, na wengine kupotezwa na wengine kuuawa. Wagombea wa upinzani wameswekwa jela, halafu utakuwaje wa haki na amani? Kama una akili timamu, huwezi kabisa kuongelea uchaguzi wa haki, kwa sababu hiyo haki mashetani yalikwishaipora zamani, kabla ya hiyo siku.

Mashetani yataenda ili yakabariki vitendo vya kishetani vya kuteka na kuua watu. Wacha mashetani yaende yakabebe laana.
 
Kuna tatizo mahala! Ukienda kituoni wewe ndio tatizo la Nchi hii
 
Makanisa nchi nzima jumapili za mwisho kuelekea uchaguzi huhamasisha waumin wao kupiga kura tena kwa Amani. Ajabu mwaka huu naona ukimia mkubwa.
 
Laana unayo wewe na ukoo wako. Kesho sisi tunatiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…