The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 3,611
- 9,269
Askofu Gwajima: Hebu CCM tumieni vichwa vyenu kufikiri na kuamua vizuri. Madai ya CHADEMA yana msingi hata kama una kiwango cha chini kabisa cha elimu kuyapima na kuyaelewa..
Askofu Gwajima: Hebu jaribu kufikiri hili. Kwamba, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya sasa ni mteule wa Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi na ni mgombea wa u - Rais. Vivyo hivyo Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume na makamishina wote watano wa hiyo Tume ni wateule wa Rais, Mwenyekiti wa CCM na mgombea u - Rais...
Askofu Gwajima: Hebu tugeuze Kibao. Kwamba, Mwenyekiti wa Tume angekuwa mteule wa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mgombea u - Rais. CCM tungekubali kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya? Nina hakika isingewezekana!
Askofu Gwajima: Kama nyie CCM msingekubali, kipi kinawafanya msione uhalali na ukweli wa dai/hoja ya CHADEMA na kurekebisha kasoro hizi ndogo tu? Kumbe mkuki ni kwa nguruwe tu, lakini kwa binadamu, mchungu siyo? CCM tupo wengi, tufanye minimal reforms, tuingie wote kwenye uchaguzi ili tuwapige vizuri. Kwanza Tundu Lissu aachiwe huru. Hakuna sababu ya kumweka gerezani hata kidogo!!
Katika hoja hii, Askofu Gwajima alimaliza kusema kwa namna hiyo...!
Soma pia PreGE2025 - Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!