Askofu Gwajima ameanza kwa kuwaambia waumini wasimame na kuimba wimbo wa 'Tanzania Tanzania', na kuongeza japokuwa tuna makabila tofauti tofauti lakini Tanzania ni yetu sote.
--
Gwajima anawaelezea waumini kuhusu mkutano wa waandishi wa habari aliofanya kuhusu suala la utekaji nchini lakini pamoja na mapendekezo aliyotoa kuhusu uteuzi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Anasema baada ya kuongea, Sheikh Jabiri huko Zanzibar alitekwa juzi tarehe 28 na mwili wake kupatikana ukiwa umetelekezwa. Watekaji wanateka MwanaCCM na watu wengine.
Chama cha Mapinduzi hakikubali utekaji, na mimi ni mwanachama wa CCM, hivyo naungana na waasisi na waliowahi kutangulia uongozi kuwa hatukubaliani na hili. Anayeteka watu ni kwa malengo yake mwenyewe. Yeyote anayepingana na mimi wenyewe mtajua mtamuitaje.
Gwajima ameongezea mifano ya watoto wa viongozi (Mwinyi, Kikwete, Majiliwa, Magufuli) ikiwa watatekwa na kung'olewa macho wazazi wao watajisikiaje?
Baada ya kukemea mauaji na utekaji, imezaliwa terminology ya Gwajimanization. "Sasa nilipoona Gwajimanization nikataka niitafasiri, hii Gwajimanization maana yake nini?" aliuliza Gwajima kabla ya kufafanua.
"Gwajimanization ama Gwajimanizing ni ujasiri usioteteleka wa kusema kweli, haijalishi ukweli huo ni mchungu au hauwapendezi walioko madarakani, ni dhamiri thabiti ya kutetea maslahi ya taifa kuliko maslahi ya mtu binafsi na kuinua sauti kwa uthubutu mkubwa bila kuyumba, kiasi cha kusababisha ivume ndani ya himaya za mamlaka na kutikisa misingi ya ufisadi na dhulma katika nchi."
Kwenye hili suala la utekaji sitayumba, nitahakikisha kila aliyetekwa anajulikana yuko wapi na anafanya nini. Vaeni silaha kamili za Bwana ili kushindana na pepo wabaya na tutashinda.
Kwa CCM, Gwajima ni hazina yenu, mnaye mtu ambaye hamjamjua bado. Ni mtu wa Mungu wa watu wote. Natetea waislam waliotekwa, Wakristo waliotekwa bila kujali chama. Kama mtu amekosea si apelekwe mahakamani. Vyombo vya ulinzi na usalama hawateki, bila shaka kunaweza kuwa na kakikundi ka utekaji na ndiko nakatumia ujumbe.
Ponjoro wa Kinondoni anachezesha kamari ambazo hata Mungu hapendi, mimi nilitaja watoto wa watu wengi ila Ponjoro kasikitika kisa mtoto mmoja niliyemtolea mfano. Nampa onyo, nikimuamkia atabaki vipande vipande na atanuka kinyesi maana mimi ni Jasusi la Mbinguni.
Naishia hapo, ila mtu akinichokoa chokoa, nitaitisha press. Na nikiitisha ya pili moshi utafuka hutoweza kufumbua macho.
Tutashusha maombi, ili damu ya mtu anayetekwa imrudie yule anayeteka.
Soma pia PreGE2025 - Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!