dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,485
Baada ya Taarifa kusambaa ya Kuvuliwa Uchungaji wa Askofu Dk Stephen Munga, ameibuka na kudai kwamba yeye bado ni Askofu.
Amedai waliomvua Uaskofu wanajifariji kwa sababu hajawahi kuitwa popote na kuhojiwa juu ya lolote. Amedai ni fitina, chuki na hila ndo zinesababisha hayo kwani Uaskofu hauvuliwi hivyo.
"Hawa ndo walisema tumekalia kuti kavu? Bado mimi ni Askofu na nimewaarifu Maaskofu juu ya hila hizo." amesema Askofu Munga.
Zaidi, soma Askofu Dk Stephen Munga wa KKKT, avuliwa Uchungaji, Wachungaji 7 Wasimamishwa