Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,935
NIWAONYE ndipo NIWAFUNDISHE
Wiki inayoishia leo 1/11/2024, kuna wezi wametumia jina langu kuandika makala wakidai naikemea CHADEMA kwa kufifisha matumaini ya watanzania. SIYO MIMI NILIYEANDIKA HIYO MAKALA. Nimegundua:
1. Jina langu linalipa. Watani zangu wa Rorya na Tarime wanaweza kulitumia kukopa mahari ya kuolea mke wa saba.
2. CHADEMA pamoja na “upumbavu” wao, ni tishio kwa walioiba jina langu na kulitumia wakidhani CHADEMA italiogopa hilo jina.
3. Watu hao wanakiharibia chama wanachokipenda na kukijenga chama wasichokipenda. Watagundua wamechelewa sana.
4. Tabia ya kutumia majina ya watu kuiba, kukopa, kutukana, kukashifu na kufitinisha haikuanza kwa kutumia jina la huyu “Askofu Mwanasiasa”. Wametumia pia iina la Padre Kitima, wazee maarufu na ninaamini wanatumia majina ya viongozi wakuu kudhuru watu na kuwatapeli kwa vyeo hewa. Kuna siku watauza nchi kwa kutumia majina maarufu.
Angalizo hili halitawazuia. Watafanya tena na hawatakemewa. Kuna siku wataomba kuhudumiwa na michepuko ya wakubwa kwa kudai wametumwa. Kama hawajafanya, wako njiani.
Novemba ni mwezi wa Watakatifu.
Iweni watakatifu ndipo mtamwona Mungu.
Sijawalaani lakini mkiendelea kuchungulia chungulia, MTAPOFUKA MACHO MJIKUTE MNAPIGA KURA PASIPOHUSIKA.
Lwakalinda.
Source: FB page yake