Kiongozi wa Kanisa wa Katoliki nchini Uingereza amesema mpango wa serikali ya Uingereza kuhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja ni jambo la aibu.
Askofu mkuu wa Jimbo wa Westminster Vincent Nichols ameiambia BBC kuwa serikali ya Uingereza haina wajibu wa kuhimiza ndoa ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uingereza.
Katika hotuba yake wakati wa ibadi ya Krismasi, askofu Nichols alisema ndoa kati ya mwanamume na mwanamke inaashiria mapenzi ya Mungu.
Serikali ya Uinbereza inapanga kuruhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja lakini imesema kuwa haitazishurutisha viongozi wa kidini kuongoza na kuidhinisha ndoa hizo.
Kwingineko, Askofu wa jimbo ya Centerbury anayeondoka, Rowan Williams amesema heshima na hadhi ya Kanisa la Kianglikana na
nchini Uingereza, limeadhirika pakubwa kutokana na uamuzi wa hivi majuzi ambao ulipinga uteuzi wa kina mama kama askofu wa kanisa hilo.
Dr Williams anatarajiwa kustaafu kutoka wadhifa huo mwisho wa mwezi huu. Askofu apinga ndoa ya wapenzi wa jinsi moja - BBC Swahili - Habari

Mheshimiwa waziri, hivi kama ni wewe ndiyo huyu askofu au shehe utafungisha ndoa wanaume wenzako kweli? Kwani ndoa si muunganisho wa mwanamme na mwanamke na si jinsia moja, au siyo? Nijuavyo mimi, mwanamme na mwanamke wanaungana kindoa ili waanzishe familia yao na si wanaume kushikishana ukuta au kina mama kushindiliana matunda ili kujipa raha. Mungu alitupa sie wanaume shamba na wanawake jembe alikuwa na maana yake. Upuuzi mwingine huu tunalazimisha tu!