Askofu amshangaa Kikwete

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,947
Askofu amshangaa Kikwete
• AHOJI KUWAGWAYA VIONGOZI MIZIGO

MWENYEKITI wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Askofu, Steven Mang'ana, ameelezwa kushangazwa na Rais Jakaya Kiktwete kushindwa kuwafukuzwa kazi viongozi wanaoonekana kuwa mzigo katika serikali yake.

Akizungumza kwenye misa takatifu ya kumsimika Mhashamu Askofu, Albert Jela Randa wa Kanisa la Mennonite (T), Dayosisi ya Mwanza, Jimbo la Nyakato jijini hapa, Askofu Mang’ana, mbali na kushangazwa na hatua kitendo hicho, pia amehoji sababu za Rais Kikwete kushindwa kuchukua maamuzi magumu, ili kuweza kulinusuru taifa.

"Madini, misitu, samaki zote zinakwenda na wawekezaji wakati serikali na viongozi wapo wa kudhibiti hali hii. Ikumbukwe kwamba, utu wa mtu haulinganishwi na kitu chochote...ee bwana waondoe hawa viongozi unaowaona ni mzigo," alisema.

Alisema kamwwe viongozi hao hawapaswi kufumbiwa mambo, kwani wamekuwa wakimwamisha maendeleo mbalimbali nchini ikiwamo kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Pamoja na hayo, alisema kuna baadhi ya wanasiasa wana tabia ya kulipiza visasi na kubainisha kuwa viongozi wa aina hiyo hawastahili kuwapo katika Tanzania ya sasa, kwani wanatishia uvunjivu wa amani nchini.

Kwa upande wake, Raish Kikwete alikiri kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya nchini na kusema serikali bado inakabiliwa na mtihani mgumu wa kudhibiti biashara hiyo haramu.

Katika kuthibitisha hayo, Rais Kikwete ameutaja mkoa wa Mwanza kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza nchini kwa biashara na matumizi ya dawa hizo, hali ambayo imemlazimu kutangaza kuunda chombo maalumu kinachojitegemea kupambana na janga hilo nchini.

Akizungumza katika misa hiyo, Rais Kikwete alisema licha ya serikali kuziunganisha Idara za Usalama: Jeshi la Wananchi (JWTZ), Polisi na Usalama wa Taifa katika kupambana na uingizwaji, utumiaji na usafirishaji wa dawa hizo za kulevya, bado mambo si shwari.

Alisema ingawa vita ya kutokomeza dawa hizo bado haijafanikiwa, mwaka jana watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara hiyo.

“Tatizo la dawa za kulevya nchini bado ni kubwa, na Mwanza ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa biashara ya matumizi ya dawa hizi.

“Niliamua kuziunganisha Idara ya Usalama wa Taifa, polisi na JWTZ katika kupambana na vita hii kwa vile kila kitengo kinawajibika kiusalama.

“Kikosi kazi hicho kipo, kinafanyakazi nzuri lakini mambo bado hayajawa mazuri, tunahitaji nguvu na ushirikiano zaidi,” alisema Rais Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika kumuweka Wakfu Askofu Randa wa kanisa hilo.

Rais Kikwete hakuishia hapo, bali aliweka wazi takwimu za dawa hizo zilizokamatwa kwa kipindi cha mwaka jana kuwa heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317.

“Kati ya gramu hizo 780, gramu 260 zilikamatwa mkoani Mwanza na watu 26 kutiwa nguvuni,” alisema bila kutaja iwapo watu hao 26 walishafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria ama la.

Katika hali nyingine, jana Rais Kikwete wakati akielekea kwenye misa hiyo ya kanisa la Mennonite alijikuta katika wakati mgumu baada ya kupokelewa njiani na makundi ya watu wengi huku wakimuonyesha alama ya vidole viwili, alama ambayo inatumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hali hiyo iliyoonekana kumshtua zaidi Rais Kikwete na msafara wake wa zaidi ya magari 20, likiwemo gari la kubeba wagonjwa (Ambulance), lenye namba za Usajili STK 8134, ilijitokeza kiongozi huyo alipofika maeneo ya stendi kuu ya mabasi Buzuruga, ambapo karibu watu wote waliokuwa wamejipanga barabarani walikuwa wakimuonesha alama ya V.


Tanzania Daima 30 Mei 2011
 
Back
Top Bottom