Askari wa usalama barabarani (traffic) na uchukuaji wa rushwa nje nje

Friday Malafyale

JF-Expert Member
Jan 18, 2017
1,808
2,911
Jana mida ya mchana nikawa napita pita zangu maeneo ya Mbagala Rangi tatu kwa miguu nikitokea Kaskazini yaani maeneo ya Dar Live nikawa napita katikati ya zile kama hifadhi ya barabara zinazotenganisha gari zinazotoka Mtoni mtongani au Posta kuja Rangi tatu na hizi gari zinazoenda Mjini tokea Mbagala Rangi tatu.

Basi mbele yangu kulikuwa na gari hizi zinazobeba mchanga wa kujengea Ikawa imesimama kuelekea kusini pale zinapoingilia daladala kuingia ndani ya kituo cha Rangi tatu.

Basi Pale kuna maaskari wengi wa usalama barabarani nnayemkumbuka sana ni huyu ana mguu mlemavu wa kushoto huwa anatembea kwa kuchechemea hivii(Hahusiki na tukio ila mwingine tuu) Basi yule dereva ikaonekana kama kuna kosa analo basi askari akang'ang'ania apewe Driving licence basi kumbe alitoa ile leseni na akaambatanisha na Elfu tano(5000 tsh) lkn Askari hakuiona basi ile dereva anaachia leseni ile 5000 ikadondoka hapo nikawa naona.

Kwa jeuri askari akajifanya kuipuuza ile hela maana watu wengi wameiona. Nikataka niwashe Camera iwe ushahidi nikaona nipotezee ila nikataka nitumie jeuri yangu nichukue ile elfu tano nione kama atafanya nini mbele ya macho ya watanzania. Nikaona aah nichaachane nazo hizo habari za ile elfu tano.

Japo wanapiga sana hizo hela ila madereva wanapigwa sana hapo Rushwa nje nje aisee.

Kazi kweli kweli Members mnakuwaga na vimaneno vya hovyo sana but ukweli ndio huo. Siku njema nia yangu sio kuchongea mtu wala
 
Kwa nini watu wanatoa rushwa na kwa nini alaumiwe traffic pekee na sio upande wa pili sisi wenyewe tukatae kutoa rushwa kukomesha hilo maake sisi pia ni sehemu ya kuzuia rushwa
 
Back
Top Bottom