figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,486
KIJANA WA MIAKA 15 APIGWA RISASI NA KUPOTEZA MAISHA NA ASKARI WA SUMA JKT WANAOLINDA MSITU WA MERU OLMOTONY NGARAMTONI WILAYANI ARUMERU
Maandamano ya wananchi wa Kijiji cha Lenjani Kata ya Lemanyata Wilayani ARUMERU yamesitishwa na jeshi la polisi wakati wakiandamana kwenda kwa mkuu wa Mkoa kutokana na kifo cha kijana mmoja ambaye alipigwa risasi kwenye msitu wa Meru Olmotony na walinzi wa Suma JKT.
Wakielezea sababu ya wao kuandamana kwenda kwa mkuu wa Mkoa wamesema kuwa ni kuchoshwa na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na askari hao wa Suma JKT ambao siyo mara yao ya kwanza kupiga watu risasi.
Akizungumza tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji cha Lenjani ambapo ndiyo kumetokea mauaji hayo Bwana Daniel Mbukuti amesema kuwa kijana huyo aliyeuwawa alikuwa anatoka mtoni kuwapa ng'ombe maji lakini wakati akipita kando kando ya msitu huo ambao unalindwa na walinzi alijikuta anapigwa risasi na kupoteza maisha wakati anapelekwa hospitalini.
Bwana Mbukuti amesema kuwa ni heri askari hao wangewakamata Mifugo na kwenda kuitaifisha kuliko kupoteza uhai wa mtoto Mdogo mdogo mwenye umri wa miaka 15 ambaye ana haki ya kuishi na kuomba serikali kushughulikia tatizo hilo ambalo ni NNE kujitokeza.
Naye diwani wa kata hiyo wa kata hiyo ya Lemanyata Bwana Losyeku Kilusu Pamoja na Diwani wa viti maalum Elinipa Musa amesema kuwa ni vema serikali ingetoa taarifa kuwa ni nani ambaye anawatuma kufanya ukatili huo wa kupoteza maisha ya watu kwasababu wananchi wake wamwekuwa wakimlaumu kuwa hafuatilii kile kinachoendelea na kijana huyo hakuuwawa ndani ya msitu huo uliopigwa marufuku wananchi Kutumia.
Naye afisa wa polisi wilaya ya Arumeru OCD Jummanne Mkwama amesema kuwa wao wanajitahidi kulinda raia pamoja na mali zake huku akiwasihi wananchi kuwa wapole kipindi hiki kigumu kwao
Chanzo cha habari ni gumzotz.