Tatizo la hao askari wanafikiri zaidi kinyama kuliko kibinadamu, ni sawa hiyo hifadhi, lakini hakuweza kutumia njia nyingine mbadala kumkamata badala ya kumuua? Wanyama ama samaki nini bwana! Na jamii inayozunguka hifadhi hiyo kubwa kuliko zote Tanzania wanafaidika katika nn? na hata huyo askari najua katekeleza tu sheria na bado analalamika mazingira ya kazi yalivyokuwa magumu. Imefikia wakati kupima kati ya samaki na binadamu yupi analeta maendeleo ya nchi, hao samaki wanahifadhiwa ili iweje na kwa faida ya nani? Inatia uchungu sana.
wasi wasi wangu ni pale watanzania watakapochukulia kwamba kufa ni kitu kidogo na cha kawaida halafu roho ya kisasi ikawaingia walah hatabaki mtu na hatakuwepo wa kuwatuliza na hata wakiwatuliza wema wao wa asili utakuwa umeshayeyuka tayari.