Askari wa JWTZ auawa kwa ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wa JWTZ auawa kwa ujambazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Dec 12, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Askari wa JWTZ auawa kwa ujambazi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 11 December 2011 21:03 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Burhani Yakub, Korogwe.
  ASKARI wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wa Lugalo jijini Dar es Salaam ameauawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira baada ya kumakamata akivunja duka la mfanyabiashara wa Kijiji cha Magamba Kwalukonge Wilayani Korogwe.

  Askari huyo aliyetambuliwa kwa jina la Amoni Kashalankolo (35) mwenye kitambulisho namba MT.83200 alikuwa katika kundi la majambazi wanne waliovamia duka la mfanyabiashara James Lomwe wakiwa na silaha aina ya SMG yenye risasi saba.Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe ni kuwa tukio hilo lilifanyika juzi saa 3 usiku katika kijiji cha Magamba Kwalukonge Wilayani Korogwe.

  Watu walioshuhudia tukio hilo walisema, majambazi hao walivamia katika duka la mfanyabiashara huyo na kumtishia kwa silaha huku wakimuamuru awape fedha za mauzo na nyingine zilizopo ambapo waliweza kupewa.

  Walisema wakati wa purukushani hiyo, familia ya mfanyabiashara huyo ilipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walipozingira nyumba yenye duka hilo ambapo mwanajeshi huyo alifyatua risasi iliyompiga
  kwenye paja mmoja wa wanakijiji waliokwenda kusaidia.

  “Katika purukushani hizo mjambazi wengine walifanikiwa kukimbia lakini wananchi waliweza kumkamata mwanajeshi huyo na kuanza kumuadhibu kwa kumpiga na baadaye wakamfunga tairi la gari shingoni na kumchoma moto,” alisema Massawe wakati akithibitisha habari hizi.

  Kamanda huyo alisema baada ya kupewa taarifa askari walikwenda kijijini Magamba Kwalukonge ndipo wakaanza kufanya msako wa kuwanasa majambazi waliokimbia.Alisema katika msako huo askari wakishirikiana na wananchi waliingia katika msitu wa karibu na kijiji hicho wakakuta pikipiki moja, nguo maalumu za kufunika nyuso pamoja na sare za jeshi la JWTZ.

  “Tupo katika msako mkali wa kufuatilia nyendo za majambazi waliotoroka baada ya kufanya tukuio hilo na tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa tutawanasa wakati wowote,” alisema Massaw[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Duh, hiyo ni kali! bado Polisi hawajikamatwi wenyewe kwa sababu wanajua namna ya kujikwepesha. Lakini mara nyingi ujambazi wa kutumia silaha unakuwa ni mpana.
   
 3. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,225
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Sio kosa lake mjeshi.ni njaa tu.si kila mtu anatafutia mkate sehem yake ya kazi?ukianza na polisi wa usalama barabarani wanapo waomba ma dereva rushwa huku wakitishiwa kupelekwa polisi. Ni sawa tu na huyo mjeshi kumtishia maisha raia uhai ili apewe chochote cha kumsaidia ktk familia yake ukizingatia wajeshi walipunguziwa kibaba chao (resheni)
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Mshaara. Mdogo . Jamani
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  mshahara wao si unakatwa na wale jamaa wa trilioni 3
   
Loading...