Askari polisi hawa hawafai

Askari polisi hawa hawafai

ericmarimbo

Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
91
Reaction score
37
Jeshi la Polisi ni moja ya taasisi zinazoheshimika sana kitaifa na kimataifa, wafanyakazi wa jeshi hili wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

Inakera na kusikitisha ninapowaona askari polisi wa kike wakiwa wamevaa sketi fupi juu kabisa ya magoti, kwa makusudi wanaonyesha mapaja yao hawa hawana tofauti na Machangudoa wanaojipitishapitisha kwa wanaume wakinadi miili yao, si polisi wa kike tu wapo pia wakiume wanavaa miligezo (kata k) tena visuruali vembamba vilivyowabana makalio, kichekesho kikubwa zaidi viatu vyao ni moka jiulize atamkimbizaje mwalifu na viatu vya moka?

IGP Mwema chukua hatua kali dhidi ya askari polisi hawa wanatia aibu. Polisi anatakiwa awe mkakamavu kuanzia kimavazi.
 
Wamezidi hawa jamaa juzi polisi huko Makete kampiga risasi mwalimu kwa kosa la kutovaa helmet,juzi hiyo hiyo Singida polisi wamempiga risasi mwananchi kwa wanachodai walizani. Ni jambazi
 
Kwanza udaili wa kujiunga jeshi haufuati viwango na maadili ya kijeshi ,undugu,ukabila unatawala sasa. Ukibahatisha kuingia jeshi bila refa umeumia hutapewa kitengo cha ela utalinda benki
pili polisi kukaa uraiani kunasababishia kushuka maadili,ulevi,ukahaba,uzinzi ,kuishiwa mshahara na kuishi kwa madeni hili ni kwa majeshi yote nchini
tatu viongozi hawaheshimiani ngazi kwa ngazi mbaya zaidi vitengo vyenye ulaji na visivyo nyeti
nne viwango vya mishahara ni kidogo ukilinganisha na maisha wanayoishi uraiani wangekuwa mess au quarters wangesitirika ndo maana wanajiingiza kwenye tabia mbaya kivitendo ujambazi,nyara ,kuuza mafuta nk
 
Mimi tangu issue ya polisi jamii ianze hata sina imani na jeshi la polisi, maans polisi wamegeuka kuwa jamii na raia
 
mkuu umeona ee mitego kila sehemu hadi chombo cha dola tatizo wahalifu wanategwa wafanye uhalifu wa kutamani wanadola.
 
nilijua unaongelea mauaji na rushwa kumbe nguo???

Hata wakitembea bila kuvaa mradi wangekuwa hawali vichwa barabarani na vituoni ingekua poa
 
Nimeona leo kwa macho yangu wale polic wanao tumia bodaboda maarufu kwajina tg wamemkamata mwendesha kibabajaji amewapa 2000
 
Wamezidi hawa jamaa juzi polisi huko Makete kampiga risasi mwalimu kwa kosa la kutovaa helmet,juzi hiyo hiyo Singida polisi wamempiga risasi mwananchi kwa wanachodai walizani. Ni jambazi

Mwema mwenyewe mdebwedo amkemee nani?
 
Mi nadhani wizara ya mambo uya ndani ifanye retrenctimement! Yaani redandas ya askari wasokwenda shule!
 
Polisi wa asa ivi ni masharobaro na mabarobaro yani uwez amin kabisa kama ni polisi kwa mavazi yao! Wanaingia upolisi kwa minajili ya kujiokoa na ugum wa maisha tu lkn si kikazi
 
Mi nadhani wizara ya mambo uya ndani ifanye retrenctimement! Yaani redandas ya askari wasokwenda shule!
kwanza nchimbi waziri wao anaitwa docta bila kupitia shula.ana degree mbili lakini anaitwa docta.sasa nani atapewa redandas kama waziri tu kafoji?
 
Mi mkuu sijali sana mavazi hoayo ni makosa kwa jeshi lao wenyewe kero langu jamaa wanakula vicha sana barabarani yaani hawathamini mshahara zaidi ya 2000 za barabarani wanakera sanaaaaaaaaaaa!
 
Maadili yapi unayoyazungumzia wewe, utendaji au mavazi?
 
Polisi ya sasa ni tofauti kabisa hatukimbizani na watu,..siku hz ni mwendo wa bata tu cha kufia nini,...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom