Askari polisi akikosea kidogo tu, anafukuzwa kazi

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
Bado naendelea kulipenda Jeshi la Polisi kwa Damu yangu yote na akili zangu zote, japo wao wananibambika kesi za mitandao na zingine zisizo na maana yoyote, mimi taendelea kuwatetea hata mkiendelea kuniweka LOKAPU au SELLO au MAHABUSU.

Polisi akipatikana na kosa liwe kubwa au dogo atawajibishwa kwa takribani mambo manne: 1. Anaweza kufukuzwa kazi mara moja, 2. Anaweza kusimamishwa kazi mara moja kwa muda, 3. Anaweza kuwekwa Sello kama adhabu na 4. Anaweza kushushwa cheo mara moja. n.k

Mimi nimejitoa Mhanga kuwatetea hawa Polisi maana najua ndani yake kuna ndugu zangu wengi tu, kuna marafiki zangu wengi tu, kuna ma classmate na ma schoolmate wangu wengi tu, kuna wanafunzi wangu wengi tu. Kwa hiyo na kwa ujumla Jeshi lote ni ndugu zangu. Nitaendelea kulitetea mpaka liwe Jeshi nazifu.

Kitabu changu kijacho cha "KOSA LA NCHI" kitalisaidia pia jeshi la Polisi kujipanga upya na kuwa imara, japo nimewasikia Chama fulani kinachonikera moyoni wakisema "Deo Kisandu tumezitumia Sera zake zote mwaka 2020 hatakuwa na sera" nasema hamniwezi, Mimi ni sawa na Biblia ukiisoma hata ukimaliza lakini bado utahitaji kufundishwa tu, AKSANTENI.

Deogratius Kisandu
Mtemi Kiongozi wa Chama cha ACA tarajiwa.
 
Mkuu Kisandu, hivi kwa sasa unajishughulisha na nini ili ukiwa unazindua ACA tuwe pamoja.
 
Kuna kosa Dogo na kosa kubwa? ha!ha!
Kama hujui kitu ni busara kukaa kimya, usijifanye unajua kitu kama Sizonje. Ni sahihi Kisandu anaposema kuna kosa kubwa na dogo na ndo maana adhabu zinatofautiana kulingana na uzito wa kosa.
 
Kuna haja ya wakuu wa idara pale SEKOM kumvua degree yake humu kiumbe.

Yaani kuzunguka kwako koooooote huko lengo lako lilikuwa moja tu,nalo ni kutangaza biashara yako ya kitabu. Haya umesomeka,bei yake itakuwa Tsh ngapi kwa kopi!?

Mi afande hapa!!

Bado naendelea kulipenda Jeshi la Polisi kwa Damu yangu yote na akili zangu zote, japo wao wananibambika kesi za mitandao na zingine zisizo na maana yoyote, mimi taendelea kuwatetea hata mkiendelea kuniweka LOKAPU au SELLO au MAHABUSU.

Polisi akipatikana na kosa liwe kubwa au dogo atawajibishwa kwa takribani mambo manne: 1. Anaweza kufukuzwa kazi mara moja, 2. Anaweza kusimamishwa kazi mara moja kwa muda, 3. Anaweza kuwekwa Sello kama adhabu na 4. Anaweza kushushwa cheo mara moja. n.k

Mimi nimejitoa Mhanga kuwatetea hawa Polisi maana najua ndani yake kuna ndugu zangu wengi tu, kuna marafiki zangu wengi tu, kuna ma classmate na ma schoolmate wangu wengi tu, kuna wanafunzi wangu wengi tu. Kwa hiyo na kwa ujumla Jeshi lote ni ndugu zangu. Nitaendelea kulitetea mpaka liwe Jeshi nazifu.

Kitabu changu kijacho cha "KOSA LA NCHI" kitalisaidia pia jeshi la Polisi kujipanga upya na kuwa imara, japo nimewasikia Chama fulani kinachonikera moyoni wakisema "Deo Kisandu tumezitumia Sera zake zote mwaka 2020 hatakuwa na sera" nasema hamniwezi, Mimi ni sawa na Biblia ukiisoma hata ukimaliza lakini bado utahitaji kufundishwa tu, AKSANTENI.

Deogratius Kisandu
Mtemi Kiongozi wa Chama cha ACA tarajiwa.
 
hahahaha sio mzima ww, Muulize Lipumba alivyopigwa na hao jamaa kama anatamani hata kuwaskia
 
Back
Top Bottom