Askari magereza atuhumiwa kulawiti raia

Askari magereza atuhumiwa kulawiti raia

mgomba101

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
1,822
Reaction score
711
Askari Magereza mwenye cheo cha koplo amenusurika kupigwa na wananchi wenye hasira, kufuatia tuhuma kwamba amewalawiti kwa siku moja vijana wawili wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 20.

Tukio la kuwalawiti vijana hao linadaiwa kufanyika kati ya saa 7.00 mchana na saa 2.00 usiku katika moja ya nyumba za kulala wageni iliyoko katika Mtaa wa Mafisa, mjini Morogoro.

Akisimulia mkasa huo, Meneja wa nyumba hiyo alisema ni desturi kwa askari huyo kwenda na vijana wa kiume katika nyumba hiyo hali iliyowatia wasiwasi wahudumu.

Alisema siku ya tukio, askari huyo alikwenda katika nyumba hiyo akiwa amempakia kijana mmoja katika pikipiki yake na kabla ya kukabidhiwa funguo ya chumba namba mhudumu wa nyumba hiyo alimweleza kuwa masharti ya nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa chumba kimoja. Alisema askari huyo alimtambulisha kijana aliyekwenda naye kuwa ni mdogo wake na kwamba walikuwa na mazungumzo muhimu.

Lakini baada ya watu hao kuingia chumbani, mmoja wa wahudumu alipita karibu na mlango wa chumba hicho na kusikia sauti ya mahaba, hali iliyomtia wasiwasi na kulazimika kuripoti tukio hilo kwa meneja wake.

Majira ya saa 11.00 jioni askari huyo alitoka na kijana huyo na kuahidi kurudi tena baadaye na aliporudi majira ya saa 1.00 usiku alirudi na kijana mwingine anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Mkoa wa Tanga.

Askari huyo alingia chumbani akiwa na kijana huyo na muda mfupi alitoka na kwenda dukani kununua kondomu na mafuta ya mgando pasipokujua kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakifuatilia nyendo zake.

Aliporudi na kuingia chumbani baadhi ya vijana waliokuwa wameandaliwa walizunguka nyuma ya chumba hicho na kuchungulia dirishani na ndipo walipojionea mambo yote yaliyokuwa yakiendelea chumbani humo.

Majira ya saa 2.00 usiku baada ya mambo hayo kumalizika kijana huyo alitoka na kumuacha askari huyo akioga. Hata hivyo kabla hajafika mbali meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa na wakazi wengine wa mtaa huo walionyesha kukerwa na kitendo kile walimvamia kijana huyo wakitaka kumhoji sababu za kushiriki kitendo cha aibu.
 
duh..machangudoa wote hawa,hivi stimu kwa mwanaume mwenzio unazipataje!!
 
Amkeni nyie mazombi, Wengi wanaolala na wanaume ni mashetani wasiojiamini ambao hawaridhiki kuwa sawa na wenzao, hivyo hutafuta wenzao wawasujudie na kuwatia ubovu (adamu alipokuwa bustanini alidanganywa na ibilisi ale tunda ili awe sawa na mungu) mfano wa tunda ni kutoa section B ukidanganywa kuwa utapewa ufalme au utajiri. matokeo yake ni kukosa hadhi. Mungu kaweka mifano katika aridhi ili tutafakari.
 
Duh!Kuna mijitu mifirauni kwenye huu ulimwengu jamani duh!Yaani kuna dhambi nyingine hata shetani anaziogopa. Kashindwa kwenda Kahumba au Itigi kuchukua changudoa mpaka anafikia uamuzi wa kishetani namna hiyo?
 
Jamaa nao naona wameamua kuja kivingine, mara mpiganaji wa JW kakamatwa na pembe za ndovu akiwa na gari la jeshi, mara vijana wa Said Mwema wamekamatwa na ''majani'' gunia 18 katika gari la polisi, duh ni balaa, lakini bora hao kuliko huyu mfiraji wa Magereza.
 
Back
Top Bottom